![]() |
Washindi katika Kongamano hilo katika mchezo wa Soka , Shule ya Msingi Murusagamba waliondoka na Zawadi ya Seti Moja ya Jezi. |
Watoto wa tarafa
ya Murusagamba wilayani Ngara mkoani Kagera wametoa ombi kwa Serikali Pamoja na Mashirika
yasiyo ya kiserikali kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ili kuondoa mila potofu
ambazo zimekuwa zikileta madhara kwa watoto mbalimbali hapa nchini pamoja na
kusimamia sheria zinazowalinda watoto.
Watoto hao
wameyasema hayo wakati wa Kongamano la watoto wa shule za msingi Tarafa ya
Murusagamba lililoambatana na michezo lililoandaliwa na Shirika la Right to
Play kwa kushirikiana na Kabanga Nikel na Halmashauri ya wilaya ya Ngara kwa lengo la kuwajengea watoto uelewa wa haki
zao na wajibu wao katika maisha yao ya kila siku.
Watoto hao wameonyeshwa
kukerwa na mila zenye kuleta madhara kwa watoto na kuitaka jamii kubadilika ili
kuziondoa pamoja na kuiomba serikali na
halmashauri kutunga sheria ndogondogo ili wale wote watakaovunja haki za watoto
waweze kuchukuliwa hatua.
Miongoni mwa
mila hizo kandamizi kwa mtoto walizozitaja ni pamoja na ndoa za utotoni,ubaguzi
wa mtoto wa kike katika familia na kufanyiwa
matendo maovu na jamii.
Aidha watoto
hao wameomba kufanyika midahalo ya mara kwa mara itakayowakutanisha watoto na
kuwasikiliza shida zao pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo katika maisha
ya kila siku na kuzitafutia ufumbuzi kwa pamoja.
Vilevile
baadhi ya watoto ambao walikuwa wakishiriki katika kongamano hilo walionyesha
kufurahishwa na mkusanyiko huo ambao Bw.Jorami Wimo yeye ni Mratibu wa Shirika
la Right to Play Tanzania Kabanga –Project amesema kongamano hilo litakuwa endelevu kwa
Wilaya ya Ngara na kwamba watoto watakuwa wakipatiwa masuala yanayohusu Afya
,Usalama barabarani pamoja na Elimu ili kuwasaidia
kufikia malengo yao.
Katika Kongamano hilo liliambatana na Michezo ambapo katika mchezo wa pete(Netball) Mshindi wa Tatu walikutana Mukubu Shule ya Msingi dhidi ya Murugunga na Mukubu kuwafunga magoli 7-3 ambapo mfungaji bora aliibuka Valalia Mvukiye huku Fainali Murusagamba Shule ya Msingi wakiibuka kidedea kwa kuwafunga Muganza magoli 9-6 na kupewa zawadi ya Seti Moja ya Jezi na Mpira.
![]() |
Mabingwa Murusagamba S/M.
|
Kwa Upande wa mchezo wa Soka ,Mshindi wa tatu aliibuka ni Ntanga Shule ya Msingi kwa kuwafunga Rwimbogo bao 3-2 kwa Maximiliani Marchades,Oscar Emanuel na Amin Jackson kuwapa ushindi wa magoli hayo Ntaga huku Magoli ya Rwimbogo yakifungwa na Filiminus Venace na Isaya Simeo.
Aidha mchezo wa Fainali wa Mashindano hayo ya Right to Play kwa shule za Msingi za tarafa ya Murusagamba,Shule ya Msingi Murusagamba waliibuka Mabingwa kwa kuwafumua Muganza bao 2-0 kwa goli za Jaston Mathayo na Dickson Pambano.
Washindi katika Kongamano hilo katika mchezo wa Soka , Shule ya Msingi Murusagamba waliondoka na Zawadi ya Seti Moja ya Jezi.
No comments:
Post a Comment