![]() |
Rio Ferdinand. |
Kabla Mechi hiyo kuanza, Rio
Ferdinand, mwenye Miaka 34 na alietwaa Ubingwa wa Uingereza mara 6 akiwa na Man
United katika Misimu yake 11, aliwekewa Gwaride la Heshima na Wachezaji wa
pande zote mbili na yeye aliingia Uwanjani akiwa na Watoto wake.
Sevilla walianza vizuri Mechi hii na
kuleta kashikashi kubwa kwa Man United na hatimae kufunga Bao 2 za haraka
zilizodumu hadi Mapumziko.
Kipindi cha Pili, Man United
waliibuka na kucheza kwa kasi na kupata Bao kupitia Valencia kufuatia kazi
nzuri ya Nyota Chipukizi Adnan Januzaj.
Mara baada ya kufunga Bao hilo,
Valencia alitoa ishara ya mapenzi na kumshukuru Mungu kwa ajili ya Straika wa
Nchi yao Ecuador, Chucho Benitez aliefariki huko Doha, Qatar Wiki iliyopita.
Baada ya hapo, Man United walikosa
Goli baada ya Goli na mwishowe Sevilla wakapachika Bao la tatu.
MAGOLI.
Man United - 1
-Valencia
Dakika ya 65.
Sevilla - 3
-Vitolo
Dakika ya 21
-Marin 25
-Rabello 91
VIKOSI.
Man United: De Gea, Fabio, Ferdinand (Evans 82), Smalling, Buttner,
Valencia (Carrick 65), Anderson (Giggs 65), Cleverley (Jones 46), Januzaj,
Kagawa (Zaha 65), Henriquez (Lingard 46)
Akiba hawakucheza: Lindegaard, Bebe, M Keane.
Sevilla: Beto, Figueiras, Fazio, Pareja (Puerto 56), Alberto, Medel,
Kondognbia, Marin, Perotti, Vitolo (Jairo 72), Bacca (Rabello 78).
Akiba hawakucheza: Julian, Navarro, Cala, Maduro, Guarente, Gameiro, Coke, Rusescu, Cotan.
![]() |
Rio Ferdinand, akiwa na Watoto wake akiwapungia mkono mashabiki wa Man United kabla ya kuanza kwa mechi na
Sevilla.
|
![]() |
Rio Ferdinand, mwenye Miaka 34, akiwapungia mkono mashabiki wa Man United
kabla ya kuanza kwa mechi na Sevilla.
|
![]() |
Kocha mpya wa United, Moyes akisaini
autographs wakati anaingia uwanjani.
|
![]() |
Vitolo akifunga bao la kwanza dakika
ya 21 pale Manchester United walifungwa Bao 3-1 na Sevilla ya Spain.
|
![]() |
Ferdinand akiwa na Rais wa Sevilla
FC, Jose Maria del Nido kabla ya mechi.
|
RIO FERDINAND-WASIFU:
JINA: Rio Gavin Ferdinand
KUZALIWA: 7 Novembar 1978, Denmark Hill, London, England
KLABU:
1992–1996 West Ham
United [Timu ya Vijana]
1996–2000 West Ham
United Mechi 127 Goli 2
1996–1997 Bournemouth
(Mkopo) Mechi 10
2000–2002 Leeds United
Mechi 54 Goli 2
2002– Manchester United Mechi 297
Goli 7
TIMU YA TAIFA:
1996–1997 England
U-18 Mechi 7
1997–2000 England U-2
Mechi 15
1997–2011 England Mechi
81 Goli 3
No comments:
Post a Comment