![]() |
For you | Ribery dedicated his "goal against Mourinho" to his boss. |
![]() |
Bayern Munich clinched UEFA Super Cup victory over Chelsea on penalties after a thrilling 2-2 draw at the Eden Arena in Prague on Friday(29,Agost 2013). |
Mabingwa
watetezi wa taji la klabu bingwa barani Ulaya Bayern Munich ya Ujerumani
wameibuka na ushindi wa taji la UEFA Super Cup baada ya kupata ushindi wa mabao
5-4 dhidi ya wapinzani wao mabingwa watetezi wa ligi ya Europa Chelsea kutoka
nchini Uingereza.
Bayern
iling'ara katika mchuano huo wa fainali uliopigwa usiku wa ijumaa kupitia
mikwaju ya penati baada ya mtanange huo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2 katika
dakika za nyongeza.
![]() |
Bayern Munich clinched UEFA Super Cup victory over Chelsea on penalties after a thrilling 2-2 draw at the Eden Arena in Prague on Friday(29,Agost 2013). |
Kiungo
wa kati wa Chelsea Ramires alitolewa nje katika dakika ya 85 baada ya kupigwa
kadi ya njano mara mbili hivyo kupelekea kikosi cha Mourinho kubakia na
wachezaji 10 pekee.
Dakika
tisini za awali zilitamatika kwa sare ya bao 1-1.
Mkwaju
ya penati ililazimika kupigwa baada ya Javi Martinez wa Bayern kupachika bao
katika dakika za lala salama hivyo kufanya sare ya mabao 2-2 katika dakika ya
121.
Ushindi
huo umekuwa ni faraja kubwa kwa Guardiola aliyechukua jukumu la kuinoa Bayern
mwezi June mwaka huu akitokea Barcelona ambapo aliiwezesha kuibuka na jumla ya
mataji 14 katika miaka yake minne ya kukinoa kikosi hicho.
No comments:
Post a Comment