Shirikisho
la kabumbu barani Ulaya UEFA limetoa ratiba ya mechi za awali za kuwania kufuzu
kukata tiketi ya kushiriki kwenye hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa
barani Ulaya, maarufu kama Champions League.
Ratiba
hiyo ambayo imetangazwa hii leo itakuwa katika mfumo wa makundi mawili yaani
kwa mfumo wa ligi na ule wa mabingwa.
Katika
zile mechi za kuwania kufuzu kukata tiketi ya kucheza klabu bingwa kupitia ligi
utazikutanisha klabu za Olympique Lyonnais ya Ufaransa itakayokuwa na kibarua
dhidi ya klabu ya Real Sociedad de Fútbol ya nchini Uhispania.
Schalke 04
ya Ujerumani yenyewe itakuwa kwenye kibarua dhidi ya timu ya FC Metalist
Kharkiv ya Ukrain, huku klabu ya Paços de Ferreira ya Ureno yenyewe itakuwa na
kibarua dhidi ya klabu ya Zenit St Petersburg ya Urusi.
Kwenye
mechi nyingine klabu ya PSV Eindhoven ya Uholanzi yenyewe itakuwa na kibarua
dhidi ya labu ya AC Milan ya nchini Italia wakati klabu ya Fenerbahçe SK ya
Uturuki yenyewe itakuwa mwenyeji wa klabu ya Arsenal FC ya nchini Uingereza.
Kwenye
hatua ya mabingwa klabu ya GNK Dinamo Zagreb ya Croatia yenyewe itawakaribisha
timu ya FK Austria Wien ya Austria huku klabu ya PFC Ludogorets Razgrad ya
Bulgaria itakuwa mwenyeji wa timu ya FC Basel 1893 ya Uswis.
Kwenye
mtanange mwingine klabu ya Viktoria Plzeň ya Jamhuri ya Czech itakuwa mwenyeji
wa timu ya NK Maribor ya Uslovania wakati timu ya Shakhter Karagandy ya
Kazakistan itakuwa mwenyeji wa klabu ya Celtic FC ya Uscotish, huku kwenye
mtanange mwingine klabu ya Steaua BucureÅŸti Romania itakuwa wenyeji wa klabu
ya Legia Warszawa ya Poland.
Katika
hatua nyingine ushiriki wa timu za Fenerbahçe SK na FC Metalist Kharkiv kwenye
hatua hii ya kukata tiketi ya kufuzu utaendelea kuwepo wakati wakisubiri uamuzi
wa kamati ya nidhamu ya UEFA.
No comments:
Post a Comment