Ni msimu wa
sikukuu ambao kimsingi unahitimisha rasmi kuondoka kwa mwezi mtukufu wa
Ramadhani. Ni wakati wa kuzichunga nafsi na kurejea kule zilikokuwa kabla ya
mfungo.
Kuondoka kwa
Ramadhan maana yake ni wafungaji walewale kujiandaa na mfungo mwingine wa siku
sita (sitashaawal) na kuanza kwa mwaka mpya wa Kiislamu.
Tukiwa ndani
ya mfungo na hata kabla mfungo haujawadia kulikuwa na maandalizi ya aina yake.
Maandalizi yalijumuisha kutafuta mavazi ya heshima na staha na yale ya ajabu
ajabu kufichwa kabisa na kuruhusu mfungo utawale.
Hadithi
zinatukumbusha kwamba kabla mfungo haujaanza sheitwani huwa anaingia kifungoni
ili kuwaepusha wafungaji na mambo yake machafu.
Ndiyo maana
ndani ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kunashuhudiwa utulivu wa hali ya
juu.
Mfungo ndio
huo unaondoka na heshima, ustaarabu, utaratibu, upole na unyenyekevu wake.
Ibilisi anaachwa
huru na kurudi ulingoni kuwapotosha wafungaji waliojinyima kwa siku hizo
walizoruzukiwa na Mwenyezi Mungu.
Haitapendeza,
si ustaarabu wala uungwana kwa mfungaji mara mwezi mtukufu unapoondoka na yeye
mara moja anarudi kwenye uchafu ambao alikuwa ameusitisha wakati wa mfungo.
Hii
inanikumbusha hadithi moja inayosema ni sawa na mtu aliyetoka kuoga na
anapomaliza anaingia tena kwenye matope na kuchafuka upya.
Ndiyo maana
Mtume (S.A.W) alisema ana hasara yule ambaye mwezi mtukufu umemdiriki na
ukaondoka akiwa hajasamehewa madhambi yake kwani kuuona au kuupata tena ni
majaaliwa yake Allah (S.W).
Kuwadia kwa
Eid hakumaanishi marejeo ya machafu tuliyokuwa tumeyaacha na tukiomba usiku na
mchana kusamehewa madhambi yake.
Itakuwa
hasara kwetu kama ilivyotajwa na Mtume (S.A.W). Tunapaswa kuzichunga nafsi na
uchafu hasa siku ya Eid Mosi na vile vile tujipange kwa Sitashaawal.
Mfungo wa
siku sita nao tunapaswa kuudiriki kwani nao una fadhila kubwa ndani yake.
Na
tukimaliza mfungo sita ndiyo mwanzo wa kujiandaa na hasa wale wenye uwezo
kwenda kufanya ibada ya kuhiji miji mitukufu ya Makkah na Madina.
Tusherehekee
Sikukuu ya Eid kama ilivyoelekezwa na Allah (S.W) na mjumbe wake Mtume Muhammad
(S.A.W).
Tumuombe
Allah atughufirie madhambi yetu na atuepushe na sheitwani muovu.
Ni sikukuu
ya kula na kunywa vilivyo halali pekee, atakaye kula na kunywa vya haramu
hakuichunga nafsi yake.
Napenda Kuwatakia Wadau wote wa Mwana wa Makonda.Blog Eid-el-Fitr njema na Kwa wale walioweza Kitimiza Nguzo Hii Muhimu ya
Kufunga Katika Mwezi Huu wa Ramadhani basi Naomba Mwenyezi Mungu azikubali
Funga zenu na Dua zote, Mwenyezi Mungu awazidishie Mema ya Duniani na Funga
zenu ziwe za Kheri,
Tushereheke
Siku kuu hii kwa Amani na Upendo, Na Kufanya yale yote yanayo Mpendeza Mwenyezi
Mungu.
Wabillahi
Tawfiq
0789 925
630/0756 830 214/0654 399 127.
No comments:
Post a Comment