![]() |
Crowds
gather on the National Mall to commemorate the 50th Anniversary of the March on
Washington, August 28, 2013.
|
![]() |
Former
presidents Jimmy Carter and Bill Clinton arrive at the Let Freedom Ring
ceremony at the Lincoln Memorial in Washington, Aug. 28, 2013.
|
![]() |
Actor Jamie
Foxx speaks during a ceremony marking the 50th anniversary of Martin Luther
King, Jr.'s "I Have a Dream" speech on the steps of the Lincoln
Memorial in Washington, August 28, 2013.
|
![]() |
A woman
stands in the crowd taking part in the anniversary of the March on Washington,
August 28, 2013. (R. Green/VOA)
|
Miaka hamsini iliyopita Mchungaji Martin Luther
King Junior aliongoza maandamano yaliyobadilisha maisha ya wamarekani wote.
Mnamo Agosti 28 mwaka wa 1963, King alitoa hotuba yake maarufu ‘ I Have a
Dream” kwa umati mkubwa wa zaidi ya watu laki mbili na nusu hapa
Washington. Tukio hilo lilibadilika kuwa la kihistoria nchini Marekani.
Watu robo
milioni waliandamana kutetea haki sawa na ajira. Maandamano hayo yalifanyika
wakati wa ghasia kubwa za ubaguzi wa rangi huku Marekani ikitafuta ufumbuzi wa
sheria zake zilizobagua wamarekani weusi
wenye asili ya Kiafrika.
Mchungaji Jesse Jackson anasema Martin Luther King alikuwa
na maono sahihi juu ya maandamano hayo
ya kihistoria.
Waliohudhuria
mkusanyiko huo wanasema ulikuwa wa
kisherehe. Wasomi wengi wa historia wanakubaliana kuwa maandamano hayo yalitoa
ujumbe mzito kwamba sharti ubaguzi wa
rangi ufike kikomo.
Mchungaji Willie Blue anasema hakutegemea tukio hilo
lingekuwa la uzito ule.
![]() |
Dr.
Martin Luther King Jr.
akitoa
hotuba Aug 28,1963
|
Dr. King
alitumia mkusanyiko huo mkubwa wa watu kutoa hotuba yake maarufu, I have a dream akieleza kuwa ana ndoto, kwamba watu
wote duniani waliumbwa sawa.
Aliashiria shida za Wamarekani weusi wakijaribu
kupigana dhidi ya ubaguzi wa rangi. Lakini
kilele cha hotuba ya Dr. King
kilikuwa pale alipoelezea kuhusu maazimio binafsi ya taifa la Marekani.
‘Nina ndoto kuwa wanangu wanne siku moja wataishi katika taifa ambalo
maamuzi juu yao hayatafanywa kwa misingi ya rangi yao, lakini kwa matendo ya
tabia zao. Nina ndoto leo”
Mbunge wa
Marekani John Lewis ambaye alizungumza wakati wa maandamano hayo, anasema
matamshi ya Dr. King yanasisimua. Alisema “Alibadili ngazi zinazoelekea kwenye
mnara wa kumbukumbu wa Lincoln kuwa kama
eneo la mchungaji anapohubiri na namkumbuka akisema nitaota leo, ndoto inayokita mizizi yake
kwenye ndoto za Marekani.”
Naye Dick
Miles alikuwa miongoni mwa wazungu wengi walioshiriki maandamano hayo.alisema
hakudhani kuna mmoja wao aliyetegemea hotuba ya kusisimua kama waliyoisikia.
‘Iligusa kila mmoja moyoni.”
Maandamno ya
Washington yalimalizika Dr. King
akiwaomba wamarekani wote wakubali uhuru utawale.
Mbunge John
Lewis anakumbuka kuwa watu walipoanza kurejea makwao, viongozi wa haki za
kiraia walikutana White House na rais John Kennedy ambaye aliwaalika White
House.
Lewis alimwelezea rais Kennedy
kama baba aliyefurahia vitendo vya wanawe; ‘alitwambia kila mmoja,
‘mmefanya kazi nzuri, na alipomfikia Dr. King, akasema ‘na wewe ulikuwa na
ndoto.”
King alisema
maandamano hayo yatakuwa mojawapo ya maandamano makubwa katika historia ya kutetea uhuru na hadhi ya binadamu kuwahi
kufanyika Marekani.
Wasomi wa historia wanasema maandamano hayo ya Washington
yalikuwa ya amani na bila shaka yoyote yalibadilisha taifa la Marekani.
![]() |
Rais Barack Obama. |
Akizungumza
na maelfu ya watu waliohudhuria maadhimisho ya miaka 50 tangu maandamano ya
kutetea haki za kiraia kufanyika jijini Washington, rais Barack Obama jana(Agosti 28,2013)
Jumatano alisema ‘kazi haijamalizika’ ya kutetea haki na usawa kwa wamarekani
wote.
Miaka 50
baada ya Mchungaji Martin Luther king
Jr. kutoa hotuba ya kihistoria na ya kusisimua akisema; “I have a dream” wakati
wa ubaguzi mkubwa wa rangi Marekani, rais wa kwanza mweusi Marekani alisimama
katika ngazi zile, zile alizosimama kwenye mnara wa kumbukumbuku wa Lincoln Memorial.
Bw. Obama
alielezea wasifu wa Dr.King pamoja na kujitolea kafara kwa walioshiriki
maandamano makubwa ya Washington miaka 50 iliyopita.
Alisema kutokana na
maandamano yao, sheria ya haki za kiraia ilipita. Na kwa sababu
waliandamana sheria ya haki za kupiga kura ilitiwa saini na kwa
sababu hiyo hiyo wasichana na wavulana weusi wanaweza kuishi maisha yao kikamilifu bila kuwa
watumwa wa mtu mwingine.
Rais Obama
aliendelea kusema na kwa sababu waliandamana, hata White House imebadilika huku
maelfu ya watu wakimshangilia. Bw. Obama alisema maandamano hayo yalileta haki
sio tu kwa wamarekani weusi lakini kwa watu wa rangi nyingine Marekani na
duniani waliokuwa na kiu cha kuwa huru.
Alisema
mengi yamebadilika tangu maandamano hayo ya mwaka wa 1963 lakini bado kuna kazi
kubwa ya kufanywa. Alisema kuna mwanya mkubwa kati ya matajiri na maskini
miongoni mwa watu wa rangi mbalimbali Marekani na migawanyiko mikubwa ya
kisiasa hapa Washington inayofanya ndoto ya Martin Luther King Jr. kuonekana
kuwa mbali sana kutimia.
Rais Obama
alisema Marekani ina chaguo, ama kuendelea na msukumo huu mkubwa wa
kidemokrasia, au kuzembea na kukifanya kizazi kijacho kuishi bila matumaini au
kujikakamua na kufanya mabadiliko ya kuleta usawa na haki kwa wote.
Orodha ya
waliotoa hotuba katika maadhimisho hayo ilikuwa ndefu, na ilijumwisha mwana wa
kike wa Dr. King, mchungaji Bernice
King, marais wa zamani Bill Clinton, Jimmy Carter, wacheza sinema maarufu na
hata watangazaji mashuhuri wa televisheni. Mbunge John Lewis mmoja wa viongozi
wa maandamano ya kutetea haki za kiraia mwaka wa 1963 alisema ingawa
kuna maendeleo, ubaguzi wa rangi ungali umejikita katika jamii ya
wamarekani.
No comments:
Post a Comment