Tazama Ngara Stars walivyoiburuza bao 3-1 Nyaishozi FC katika uwanja wao wa Nyumbani. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, August 23, 2013

Tazama Ngara Stars walivyoiburuza bao 3-1 Nyaishozi FC katika uwanja wao wa Nyumbani.

Hiki ni kikosi cha Kwanza cha Ngara Stars ya Mjini Ngara  kilichoanza mchezo dhidi ya Nyaishozi FC ya Kata ya Nyaishozi ,wilayani Karagwe mkoani Kagera na kuifunga mabao 3-1 katika uwanja wao wa Nyumbani (Agosti 18,2013),magoli ya Ngara Stars yakifungwa na Fadhir Kijanjar,Fadhir Rashid na Salumu a.k.a Fundi Mativi huku goli la Nyaishozi FC likifungwa na Camilius Kikwato.

Kikosi cha Kwanza cha  ya Nyaishozi FC ya Kata ya Nyaishozi ,wilayani Karagwe mkoani Kagera  kikiwa katika picha ya pamoja na kilichocheza na Ngara Stars ya mjini Ngara  mchezo wao wa kirafiki wa kiujirani mwema baina ya timu hizo mbili.


Benchi la wachezaji wa akiba la Ngara Stars ya mjini Ngara mkoani Kagera .



Mashabiki wakifatilia mchezo kati ya  Ngara Stars  dhidi ya Nyaishozi FC ambayo ilikubali kufungwa mabao 3-1 katika uwanja wao wa Nyumbani wa Nyaishozi.

Mgogoro ukazuka na mchezo kusimama kwa dakika 5 baada ya refari mwenye kibagarashia kichwani kushindwa kutafasiri vyema sheria 17 za mchezo wa soka uwanjani.

Viongozi wa timu ya Ngara Stars Baraka Abas kushoto na mwenzake  kulia wakitoka uwanjani mara baada ya kusuluhisha zogo lililosababishwa na mwamuzi wa mchezo huo kutoa maamuzi ya utata dhidi ya Ngara Stars yaliyopelekea wachezaji  kumlaumu kila wakati wa mchezo.

Benchi la wachezaji wa akiba la Nyaishozi FC ya Kata ya Nyaishozi ,wilayani Karagwe mkoani Kagera .


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad