Tazama hali halisi ya Uboreshaji Elimu wilayani Ngara mkoani Kagera ilivyo bado ni Changamoto. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 24, 2013

Tazama hali halisi ya Uboreshaji Elimu wilayani Ngara mkoani Kagera ilivyo bado ni Changamoto.

Muonekano Juu na Chini wa Wanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera wakiwa darasani kwa kukalia vigoda baada ya kukosa madawati shuleni hapo....Picha na Shaaban Ndyamukama.



Wanafunzi wa kiume shule ya msingi Rulenge wilayani Ngara wakiwa katika foleni ya kupata huduma ya choo katika matundu yenye milango.

Wanafunzi wa shule ya msingi Rulenge wilayani Ngara wakiwa katika foleni ya kufanya usafi wa vyoo vilivyojaa huku  wanafunzi wenzao wakisaidia  ovyo na kuharibu mazingira.

Vyoo vya shule ya msingi Rulenge vikiwa baadhi yake havina hata milango na wanafunzi kuogopa kuvitumia wakihisi kupata magonjwa ya mlipuko.
Na Shaaban Ndyamukama.

Idara ya elimu katika Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera imeweka mpango mkakati wa  kufaulisha wanafunzi wa darasa la saba kwa asilimia 90 katika mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi inayotarajia kuanza Septemba 11 na 12 mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na  Afisa elimu wilayani Ngara Bw Simon Mumbee wakati akiongea na Mwandishi wa Habari hizi ofisini kwake kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Big Results Now iliyowekwa na   waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dr. Shukuru Kawambwa   hivi karibuni  jijini Dares Salaam.

Bw Mumbee alisema kiwango cha asilimia hizo ni kutoka asilimia 70 katika miaka minne iliyopita kwani changamoto kubwa ya  vitendea kazi  hasa vitabu kwa walimu na wanafunzi imepungua baada ya serikali kutoa vifaa hivyo.

 Aidha alisema katika kutekeleza maazimio hayo walimu na wanafunzi watakaokuwa katika ufaulu mzuri watapata motisha mbali mbali ili kuwajengea uwezo wa kujituma katika kutekeleza na kutimiza majukumu yao.

“Haya ni malengo ya wilaya na mkoa mzima wa kagera na jambo muhimu ni kuhakikisha walimu wanafundisha kwa kuzingatia mihtasari ya masomo kwa kuwa na maandalio ya kila siku na maazimio ya kazi huku wakiingia darasani kufundisha”.Alisema Mumbee.

Wakati mikakati hiyo ikiwekwa na idara hiyo,Uhunguzi wa Mwanawamakonda Blog, imebaini wanafunzi wa shule ya msingi Rulenge mjini wilayani Ngara wanaosoma  darasa la kwanza na la pili wakijifunza kwa kukalia vigoda kwa  kukosa madawati.
 
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Mashaka makemba amesema kuwa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1374 na serikali ya kijiji ilikuwa na mpango wa kujenga shule mpya
Alisema kuwa changamoto nyingine ni wanafunzi wa shule hiyo kukosa huduma ya vyoo kwani vilivyopo vimejaa huku wanafunzi wa elimu ya awali hadi darasa la tatu wakijisaidia ovyo na  kuchafua mazingira.

Hata hivyo alisema juhudi za kujenga shule mpya ili kupata vyumba vya madarasa pamoja na matundu ya vyoo zimegonga mwamba baada ya  ardhi iliyolengwa kuwekwa shule kuwa na  mgogoro kati ya serikali ya kijiji na Mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoani Kagera Pius Ngeze anayedai kuwa na hati miliki ya eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad