![]() |
Viungo
Vinavyosafisha Mwili (kiingereza Excretory Organs) ni viungo
katika mwili wa binadamu ambavyo
vinahusika katika utoaji wa taka mwilini. Binadamu kama viumbe haiwengine wanahitaji kutoa uchafu.
Hakuna mfumo maalumu katika mwili wa binadamu ambao unahusika moja kwa moja katika
utoaji wa uchafu kama vile kwa mfano mfumo
wa upumuaji ambao unahusika moja kwa moja na upumuaji.
Viungo mbalimbali kutoka katika mifumo
mengine kwa pamoja huweza kufanikisha suala la kusafisha mwili.
Mfano viungo kama mapafu, mafigo na ngozi ambavyo
vipo katika mifumo mengine hutumika katika mpangilio uliotajwa kutoa hewa
chafu, mikojo na jasho.
Viungo hufanya kazi zingine pia zaidi ya utoaji taka, kwa mfano ngozi pia
huhusiaka katika kutunza joto la mwili na kadhalika.
Viungo hivi kwa pamoja hata kwa kuwa sehemu
mbalimbali katika mwili wa binadamu kwa pamoja huwekwa katika mfumo
wa utoaji taka.
Utangulizi
Wanadamu hula chakula na kunywa maji kwa
sababu miili yao hupaswa kulishwa ili isidhoofike wala kuwa na afya mbaya.
Lakini katika chakula na maji zimo sehemu nyingine za vitu hivi zisizotufaa, na
hizi sehemu lazima zitengwe na kutolewa nje ya miili. Kama sehemu hizo
hazitolewi tutapatwa na magonjwa na
hatimaye tutukufa.
Mapafu
Kila kiumbe hai kinahitaji
hewa ya oksijeni ili kiweze kuishi. Kila kiumbe
kina namna ya kujipatia hewa hii muhimu kwa uhai.
Halikadhalika wanyama jamii ya mamalia hujipatia hewa kwa kutumia mapafu. Binadamu ana mapafu
mawili yaliyo ndani ya kifua.
Binadamu hutumia hewa ya oksijeni katika
kujitengenezea nishati kutoka katika
chakula kwa ajili ya matumizi mbalimbali mwilini. Miongoni ya matokeo ya pambano la
chakula na oksijeni pamoja na vimeng’enyo mbalimbali
ndani ya seli ya binadamu, pamoja na vitu vingine
ni hewa ya carbondioxide.
Hewa hii husafirishwa katika damu mpaka ndani ya
mapafu ambao huitoa nje kama uchafu
ndani ya mwili.
Kiwango cha hewa ya carbondioxide kinachotolewa nje
kila mtu anapopumua kinaweza kufikia asilimia nne au zaidi ya hewa yote
inayotolewa nje. Zaidi ya hayo mapafu hutoa maji mengi kwa namna ya mvuke.
Ini
Ini ni miongoni mwa ogani muhimu katika mwili
wa binadamu.
Pia ini ni mojawapo ya viungo vinavyohusika katika kutoa uchafu.
Ini hutumika pia katika uhifadhi wa chakula katika mwili wa binadamu.
Chakula
kinapofonjwa kuingia mwilini katika utumbo mwembamba huelekea kwanza katika
ini. Ini husafisha sumu katika mwili. Kunapokuwa na uongezeko la chakula cha
protini, ni jukumu la ini kurekebisha.
Uchafu unaotolewa na ini huingizwa
katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na hutolewa pamoja na kinyesi.
Mfumo
wa mkojo
![]() |
Mafigo |
Katika mwili wa binadamu mafigo yamewekwa
nyuma ya tumbo; moja kwa kila upande wa pingili za juu
za kiuno.
Sehemu ya juu ya mafigo imehifadhiwa
kwa jozi mbili za mbavu zinazoelea.
Kila figo kwa umbo lake hufanana na haragwe,
lakini kwa ukubwa ni tofauti sana. Figo la kulia kwa kawaida ni fupi na nene
zaidi, nalo, kwa sababu ya ini, hukaa chini zaidi kuliko
figo la kushoto.
Mafigo yametengenezwa yawe mfano wa chombo
cha kuchujia maji. Kazi yake ni kuchuja maji na kutoa uchafu na vitu vyote
visivyohitajika mwilini vilivyochukuliwa na damu katika
safari zake.
Maji hayo pamoja na vitu hafifu vilivyomo ndiyo mkojo.
Mafigo yameshehenezwa na vifereji vilivyonyongwanyongwa, navyo vyote huunganika
pamoja kufanya bomba lile litokalo katika kila figo na kufika mpaka katika kibofu
cha mkojo.
Kibofu cha Mkojo
Kibofu ni mfuko wa mkojo uliopo mvunguni mwa
matumbo. Kwa hiyo mkojo hauwezi kutoka mojamoja mara tu unapotengenezwa na
mafigo.
Kibofu kinapojaa mkojo, mtu huhisi haja ndogo.
Kiasi cha mkojo unaotolewa kila siku hubadilika siku hadi siku. Hii hutegemea
na hali mbalimbai. Mtu mwenye afya njema hutoa lita moja na nusu hadi lita
mbili na nusu za mkojo katika muda wa masaa 24.
Kiasi cha mkojo, huongezeka kama mtu amekunywa sana vinywaji, kwa mfano, pombe, divai, maji
ya machungwa au mananasi, au kama amepatwa na magonjwa
ya figo. Hapa mkojo huwa si wa manjano sana.
Kiasi cha mkojo unaotolewa kila siku hupungua kama mtu hakunywa sana kinywaji
cho chote au kama ametokwa na jashosana.
Hali hiyo hutokea pia mtu ashikwapo na homa.
Hapo mkojo huwa na rangi ya kimanjano sana, pengine ni wa hudhurungi,
na pengine hatakikahawia.
Ngozi
Sehemu ya nje ya mamalia imefunikwa na ngozi.
Kutegemeana na mamalia kiwango cha nywele kinachoweza kutoa juu ya ngozi kinategemea
asili au mahali ambapo mamalia anapatikana. Ngozi ya binadamu inaweza kuwanywa
katika sehemu mbili; nazo ni ngozi ya ndani na ngozi ya nje.
Ngozi ya Nje
Ngozi ya
nje ni matabaka mengi ya magamba. Ngozi inaposuguliwa magamba haya
hutoka. Hayo yanaonekana katika ngozi ya kichwa.
Matabaka ya chini hayana magamba mengi nayo huwa na
rangi maalum ionekanayo katika mataifa makuu ya jamii
ya wanadamu. Ngozi ya nje hulinda sehemu za mwili zilizo chini yake
na ambazo zina kapilari.
Kwa hiyo mtu asiye na ngozi iliyochubuka anaweza kugusa na kutumia vitu vya
maji maji vilivyo na sumu naye asidhurike
navyo.
![]() |
Ngozi ya ndani
Ngozi ya
ndani au ngozi
halisi iko chini au baada ya ngozi ya nje. Ndani ya ngozi ya
ndani vimo vinyweleo
vya jasho vingi visivyoweza kuhesabika.
Karibu na vinyweleo
hivyo zipo kapilari.
Kila kinyweleo kimefanana na kifereji kilichonyongwanyongwa, na katika kuta
zake vimo vifuko vidogo sana kama vile vilivyomo katikamafigo.
Vifuko hivyo vinaweza kuondoa uchafu uliomo
katika damu na kuupitisha katika vinyweleo mpaka
kuutoa nje ya ngozi. Kwa kawaida jasho huwa
halionekani kwa sababu linatoka kwa namna ya mvuke na hutolewa katika hewa.
Hapo huitwa jasho
lisiloonekana, lakini tukifanya kazi ngumu
au kutikiwa na jotosana,
basi hapo huwa tunatoa jasho linaloonekana wazi wazi.
Zaidi ya vinyweleo viko pia vitundu vidogo
vingi sana vya malaika, na kila kutundu
kina laika yake. Katika vitundu hivyo yamo mafuta, na kazi yake ni kulainisha ngozi isiwe ngumu wala
isipasuke kwa baridi.
Kazi ya ngozi
Kimsingi ngozi ina kazi mbalimbali. Kwa
ufupisho baadhi yake ni kama ilivyofupishwa hapa chini-
·
Kutupatia mlango
wa maarifa yaani kugusa.
·
Kusafisha mwili kwa kutoa nje ya mwili vitu
vyote vichafu na visivyohitajika.
·
Kusawazisha joto la
mwili.
·
Kulinda kapilari na
sehemu zingine zilizomo ndani ya mwili.
Hitimisho
Utoaji uchafu katika mwili ni moja kati ya
sifa ya msingi ya kiumbe hai.
Inapasa mwili wa kiumbe hai uwe katika uwiano sawa ili uweze kufanya kazi kwa afya bora na
kuongezamuda wa
kuishi.
Sumu na uchafu ndani ya mwili husababisha kutofanya kazi
vizuri na hivyo kusababisha baadhi ya sehemu mbalimbali za mwili kufa mapema.
Afya bora hasa katika ulaji wa mlo kamili vinasaidia
kwa kiwango kikubwa katika uboreshaji wa viungo hivi muhimu katika kusafisha
mwili mzima wa binadamu kwa ndani.
Dhamana ya kusafisha mwili kwa nje kama vile
kuuosha kwa maji na kuondoa uchafu unaoachwa nje ya mwili (mfano jasho) na
viungo vya ndani, imeachwa kwa kiumbe chote kwa ujumla. Hivyo umetupasa kutunza
miili yetu kwa kuiosha kila wakati inapochafuka.
Sorce:Wikipedia.
No comments:
Post a Comment