Robin Van Persie aiwezesha Manchester United kuilaza 2-0 Wigan kwenye Uwanja wa Wembley na kutwaa Ngao ya Jamii. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 11, 2013

Robin Van Persie aiwezesha Manchester United kuilaza 2-0 Wigan kwenye Uwanja wa Wembley na kutwaa Ngao ya Jamii.

Wachezaji wa Manchester  United wakimpongeza Van Persie baada ya kufunga bao la kwanza  katika ushindi wa mabao  2-0  dhidi ya Wigan kwenye Uwanja wa Wembley na kutwaa Ngao ya Jamii leo(Agosti 11,2013).


Robin van Persie akipiga kichwa kuifungia Manchester United bao la kwanza dhidi ya Wigan kwenye Uwanja wa Wembley na kushinda Man united bao 2-0 kutwaa Ngao ya Jamii leo(Agosti 11,2013).


Winga mpya wa Man United, Wilfried Zaha akimtoka Ben Watson katika mchezo huo wa Ngao ya Jamii.

David Moyes na Owen Coyle wakiwapigia kelele wachezaji wao kuwapa maelekezo katika mchezo huo wa Ngao ya Jamii ambao Man United waliibuka na ushindi wa mabao  2-0  dhidi ya Wigan kwenye Uwanja wa Wembley na kutwaa Ngao ya Jamii leo(Agosti 11,2013).


Van Persie akiifungia Manchester United bao la pili  dhidi ya Wigan kwenye Uwanja wa Wembley na kutwaa Ngao ya Jamii leo(Agosti 11,2013).
Magoli  mawili ya Mholanzi  Robin Van Persie yameiwezesha Manchester United kuilaza 2-0 Wigan kwenye Uwanja wa Wembley na kutwaa Ngao ya Jamii.

Ushindi huo ni faraja na mwanzo mzuri kwa kocha mpya wa United, David Moyes aliyerithi mikoba ya Sir Alex Ferguson aliyestaafu mwishoni mwa msimu uliopita. 

Van Persie alifunga bao la kwanza dakika ya saba kwa kichwa cha nguvu, akiunganisha krosi ya Patrice Evra kutoka wingi ya kushoto na akafunga la pili dakika ya 59 baada ya kufumua shuiti lililombabatiza beki wa Wigan, James Perch.

Kikosi cha Man Utd kilikuwa: De Gea, Rafael/Smalling dk16, Jones, Vidic, Evra, Zaha/Valencia dk61, Carrick, Cleverley, Giggs/Anderson dk67, Welbeck/Kagawa dk83 na Van Persie/Januzaj dk84. 


Wigan: Carson, Boyce, Perch, Barnett, Crainey, McCarthy/Dicko dk86, Watson/Espinoza dk71, McArthur/McCann dk61, Maloney/Gomez dk71, Holt/Fortune dk61 na McClean/McManaman dk62. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad