Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda yupo chini ya ulinzi huku akitibiwa majeraha katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Sheikh
Ponda alisafirishwa usiku wa manane kutoka Morogoro baada ya juzi kupigwa na
kitu kinachodaiwa kuwa ni mtutu wa bomu saa 12:25 jioni alipokuwa akisindikizwa
na wafuasi wake kwenda katika Msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja mara baada ya
kumaliza kutoa mhadhara katika kongamano mjini hapo.
Hata
hivyo, Mwenyekiti wa Kongamano hilo, Sheikh Idd Mussa Msema, alidai kuwa Sheikh
Ponda alipigwa risasi tatu begani.
Taarifa
kutoka ndani ya familia ya Ponda zilisema kwamba baada ya kupata taarifa za
kupigwa risasi, baadhi ya masheikh walifunga safari kwenda Morogoro na
kumrejesha Dar es Salaam usiku huohuo.
Kabla
ya kurudishwa Dar es Salaam, imeelezwa kuwa Sheikh Ponda alipelekwa katika
Zahanati ya Islamic Foundation.
Mmoja
wa wanafamilia alidokeza kwamba Sheikh Ponda alifichwa na alikuwa chini ya
ulinzi mkali wa wafuasi wake na hakuna aliyeruhusiwa kumsogelea.
Hata
hivyo, habari zilizopatikana baadaye jana(Agosti 11,2013) zilisema kuwa alifikishwa Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Sheikh
Ponda alifikishwa Muhimbili jana saa 7:18 mchana na alipelekwa kwenye chumba
cha wagonjwa wa dharura na baadaye alitolewa na kupelekwa kwenye chumba cha
x-ray kwa ajili ya vipimo. Baadaye alipelekwa chumba cha upasuaji.
Eneo
kubwa la hospitali hiyo lilikuwa na idadi kubwa ya askari na mmoja wa askari
waliokuwa doria hospitalini hapo alisema walitawanywa kwenye hospitali
mbalimbali za Dar es Salaam baada ya kupata taarifa kuwa angeletwa kwa
matibabu.
“Nakuambia
tuko hapa tangu saa kumi na moja asubuhi, tumetawanywa hospitali mbalimbali
baada ya kupata taarifa kuwa analetwa Dar. Bahati nzuri kaletwa hapa
Muhimbili... tunasubiri apate matibabu na tutamtia mbaroni,” alisema askari
huyo.
Taarifa ya Jeshi la Polisi
Msemaji
wa Polisi, Advera Senso alisema jana katika taarifa yake kuwa Sheikh Ponda yuko
Hospitali ya Muhimbili akitibiwa baada ya kupata majeraha yaliyotokana na
purukushani na polisi wakati wafuasi wake walipokuwa wanataka kumtorosha.
Sorce:Mwananchi.
No comments:
Post a Comment