![]() |
Wachezaji wa Manchester United wakimpongeza Van Persie baada ya kufunga bao la kwanza katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wigan kwenye Uwanja wa Wembley na kutwaa Ngao ya Jamii leo(Agosti 11,2013). |
![]() |
Robin van Persie akipiga kichwa kuifungia Manchester United bao la kwanza dhidi ya Wigan kwenye Uwanja wa Wembley na kushinda Man united bao 2-0 kutwaa Ngao ya Jamii leo(Agosti 11,2013). |
![]() |
Winga mpya
wa Man United, Wilfried Zaha akimtoka Ben Watson katika mchezo huo wa Ngao ya
Jamii.
|
![]() |
Van Persie
akiifungia Manchester United bao la pili dhidi ya Wigan kwenye Uwanja wa Wembley na
kutwaa Ngao ya Jamii leo(Agosti 11,2013).
|
Magoli mawili ya Mholanzi Robin Van Persie yameiwezesha Manchester
United kuilaza 2-0 Wigan kwenye Uwanja wa Wembley na kutwaa Ngao ya Jamii.
Ushindi huo ni faraja na mwanzo mzuri kwa kocha mpya wa United, David Moyes aliyerithi mikoba ya Sir Alex Ferguson aliyestaafu mwishoni mwa msimu uliopita.
Van Persie
alifunga bao la kwanza dakika ya saba kwa kichwa cha nguvu, akiunganisha krosi
ya Patrice Evra kutoka wingi ya kushoto na akafunga la pili dakika ya 59 baada
ya kufumua shuiti lililombabatiza beki wa Wigan, James Perch.
Kikosi cha
Man Utd kilikuwa: De Gea, Rafael/Smalling dk16, Jones, Vidic, Evra,
Zaha/Valencia dk61, Carrick, Cleverley, Giggs/Anderson dk67, Welbeck/Kagawa
dk83 na Van Persie/Januzaj dk84.
Wigan: Carson,
Boyce, Perch, Barnett, Crainey, McCarthy/Dicko dk86, Watson/Espinoza dk71,
McArthur/McCann dk61, Maloney/Gomez dk71, Holt/Fortune dk61 na
McClean/McManaman dk62.
No comments:
Post a Comment