Kamanda Leonard Paulo-Geita. |
JESHI la
polisi mkoani Geita limemfikisha mahakamani Bi,Sophia Ngeleja (65) mkazi
Butundwe wilayani Geita anayedaiwa kukamatwa akiwa uchi wa mnyama nyumbani kwa
Bahabi Shomari (30) mkazi wa kijiji Mkuyuni wilayani Chato August 4 majira ya
saa 03:00 usiku.
Mtuhumiwa Sophia
Ngeleja alisomewa shitaka lake katika mahakama ya wilaya ya Chato August 5
mwaka huu na mwendesha mashitaka wa polisi,mkaguzi msaidizi wa polisi,Mkwasi
Rashidi mbele ya hakimu mkazi mfawiidhi wa mahakama ya
Chato,Bw.Jovith Katto.
Mwendesha
mashitaka alidai kuwa mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa la kujihusisha na vitendo
vya kishirikina August 4,majira ya saa 03:00 usiku nyumbani kwa Bahabi
Shomari,mkazi wa kijiji cha Mkuyuni wilayani Chato,ambaye pia ni mtumishi wa
Halmashauri ya wilaya ya Chato ambapo siku ya tukio alikutwa akiwa uchi wa
mnyama kitendo ambacho ni kinyume na sheria ya uchawi no.18 kifungu cha 3 na 5
ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho.
Kwa mujibu
wa mwendesha mashitaka alidai kuwa mtuhumiwa alipelekwa Hosptali ya wilaya ya
Chato kufanyiwa uchunguzi wa afya yake,ambapo uchunguzi wa kitabibu
ulithibitisha kuwa afya na akili za mwanamke huyo ni timamu.
Mtuhumiwa
alikana kosa na kupelekwa gerezani Biharamlo,baada ya kushindwa kutimiza
masharti ya dhamana,ampo kesi hiyo imehairishwa hadi August 19 itakapotajwa
tena.
ALIVYOKAMATWA.
Siku ya
tukio August 4,majira ya saa tisa usiku,Shomari Bahabi akiwa nyumbani kwake
amelala alisikia kishindo cha mtu nje katika mlango wa nyumba yake wa
mbele,baada ya hapo alichungulia nje na kumuona mtu akiwa nje huku akiwa uchi
“nilikuwa naona kama naota ila niliamua kufungua mlango wa nyuma na kukimbia
kwa mwenyekiti wangu wa kitongoji Bw.Kadri Mohamed ambaye pia ni jirani yangu
nilikuja naye hadi pale kwangu na kumkuta Yule mama akiwa amenasa
mlangoni,tuliwaamsha na watu wengine usiku huo” alieleza Bahabi
“baada ya
kumhoji alidai alikuwa yeye ni mkazi wa Butundwe wilayani Geita na
alikuwa na wenzake nane ambao wamemuacha,alikuwa anaongea
kwa ujasri pengine husingeamini,watu walizidi kuongezeka maana hapa kwangu ni
njiani hata hivyo walikuwa wakipashana habari na kila mtu alitaka
ashuhudie,tulikaa naye hadi saa 06:30 asubuhi polisi wa Chato walipokuja
kumchukua,wakati wote huo alikuwa uchi”aliongeza.
Kwa upande
wa mwenyekiti wa Kitongoji Bw.Kadri Mohamed alidai kwake ni tukio la kwanza na
matukio hayo alikuwa akiyasikia mikoa mingine ila hakuwahi kuamini hadi
lilipotokea kwenye kitongoji chake” siku hiyo saa tisa wakati Shomari
ananiamsha sikuamini nilifikiri amechanganyikiwa hadi nilipofika kwenye tukio
na kumkuta mtu akiwa uchi” anasema kwa kusikitika.
“nilipofika
nilimuuliza jina lake maana hapa kijijini alikuwa ni mgeni,ndipo aliposema
kwamba yeye ni Sophia Ngeleja na ni mkazi wa Butundwe,na kwamba alikuwa na
wenzake nanae wamemuacha hivyo anaomba msamaha,sikuwa na la kufanya zaidi ya
kupiga simu polisi maana nilijua wananchi wanaweza kumdhuru,polisi walifika na
gari ndogo na kuondoka naye akiwa hana nguo”aliongeza Mwenyekiti wa kitongoji.
Aidha mmoja
wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alidai
kuwa mama huyo hakupigwa kutokana na kwamba kila mmoja aliyefika pale kuingiwa
na hofu.
”yaani mimi
mwenyewe nilikuwa natetemeka maana ulikuwa kama muujiza ama mazingaombwe”
alidai shuhuda huyo.
Na:Denice Stephano-Geita.
0767925018
No comments:
Post a Comment