Mtu mmoja amefariki Dunia na wengine 15 wamejeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Hood lililokuwa likitokea wilayani Kilombero kwenda jijini Dar es salaam kumgonga mtembea kwa miguu na kisha kuacha njia na
kupinduka katika eneo la Kiembeni Mikese
Mkoani Morogoro.
Mkuu wa
kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro Bw. Bonifasi Mbao akizungumza kwenye eneo la tukio leo(Agosti 28,2013) amesema
chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi
ambapo dereva wa basi gari ilimshinda na kugonga mtembea kwa miguu na
kisha kupinduka ambapo dereva wa basi
amekimbia mara baada ya tukio la ajali.
![]() |
Basi la Kampuni ya Hood likiwa limeacha njia na kupinduka katika eneo la Kiembeni Mikese Mkoani Morogoro baada ya kumgonga mtembea kwa miguu leo (Agosti 28,2013) |
Taarifa
za madaktari katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro zimeeleza
majeruhi wanaendelea na matibabu na mwili wa marehemu umehifahiwa katika
chumba cha maiti hospitali ya mkoa wa Morogoro .
Chanzo Na: ITV
No comments:
Post a Comment