Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania, TCRA Jana(Agosti 28,2013) imevifungulia vituo vya
utangazaji vya Radio Imaan ya mjini Morogoro na Kwa Neema FM Radio ya jijini
Mwanza vilivyokuwa vimefungiwa kwa miezi sita kutokana na kukiuka Sheria na
Kanuni za Utangazaji.
Uamuzi
wa kuvifungia vituo hivyo ulichukuliwa tarehe 26/02/2013 na Kamati ya Maudhui
ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
Taarifa
hiyo imetolewa leo na TCRA kupitia taarifa kwa vyombo vya habari.
Mnamo
tarehe 26/02/2013 Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilitoa
uamuzi wa kuvifungia vituo vya utangazaji vya Radio Imaan ya mjini Morogoro na
Kwa Neema FM Radio ya jijini Mwanza baada ya kukiuka Sheria na Kanuni za
Utangazaji.
Kamati
ya Maudhui iliuita uongozi wa vituo hivyo tarehe 11/02/2013 na tarehe 14/02/2013
ili kujitetea na vyote vilikiri kosa.
Baada
ya kutafakari utetezi wa Radio Imaan na Radio ya Kwa Neema FM na kwa kuzingatia
Sheria na Kanuni za Utangazaji, Kamati iliamua kutoa adhabu kwa vituo vyote
viliwi kama ifuatavyo:-
a)
Vituo vyote vilipewa onyo pamoja na kufungiwa kurusha matangazo kwa kipindi cha
miezi sita kuanzia tarehe 26/02/2013;
b)
Vituo vyote vilitakiwa kuithibitishia Mamlaka ya Mawasiliano na Kamati ya
Maudhui kwa maandishi kuwa hawatarejea kutenda kosa la aina hiyo au linalofanana
na hilo. Ikiwa vitarudia Kamati ya Maudhui haitasita kuvifutia leseni zao za
utangazaji.
Kutekeleza
adhabu na hatua zilizochukuliwa na vituo hivyo na Mamlaka ya Mawasiliano:
Baada
ya Uamuzi huo kusomwa, vituo vyote viwili vilianza kutekeleza adhabu mara moja
kama ilivyotakiwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utangazaji.
Mamlaka
ya Mawasiliano ilipokea barua ya udhibitisho wa kutofanya kosa tena yaani
pamoja na sera ya uhariri (Editorial Policy) na ratiba ya vipindi kutoka kwa
vituo vyote viwili.
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania ilifanya ukaguzi kwa vituo vyote viwili ili
kujiridhisha na kuzipitia sera za uhariri pamoja na mwongozo wa vipindi kabla
ya kuvifungulia.
Kurejeshwa
kwa Matangazo*
Kamati
ya Maudhui iliandika barua tarehe 27/08/2013 kuhusu kuvifungulia vituo hivyo
vya utangazaji vya Radio Imaan ya mjini Morogoro na Kwa Neema FM Radio ya
jijini Mwanza baada ya kutumikia adhabu kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za
Utangazaji.
Vituo
hivi vimeanza kurusha matangazo yake kuanzia leo tarehe 28/08/2013 baada ya
muda wa adhabu kuisha.
Kamati
ya Maudhui inapenda kutumia fursa hii kuvionya vyombo vya habari vya utangazaji
vya redio na televisheni kuwa makini katika kutekeleza masharti ya leseni
pamoja na kufuata Sheria na Kanuni za Utangazaji.
Kamati
ya Maudhui haitasita kutoa adhabu kali au kuvifungia vituo vitakavyokiuka
Masharti ya leseni, Sheria pamoja na Kanuni za Utangazaji au hata kuvifutia
leseni zao.
Kamati ya Maudhui inatoa wito kwa vyombo vya habari vya utangazaji
kuzingatia Sheria, Kanuni na Masharti ya leseni ilikuboresha Sekta ya
Utangazaji na kudumisha amani nchini.
Eng.
Margaret Munyagi
Mwenyekiti,
Kamati
ya Maudhui Ya TCRA,
S.L.P.
474,
DAR
ES SALAAM
No comments:
Post a Comment