Waliooa |
Wanaume
waliooa wanawake wenye mishahara mikubwa au vyeo kuwazidi wao, huathirika
kisaikolojia wakati wa tendo la ndoa na wengi wao hutoka nje ya ndoa. Utafiti
umebaini.
Utafiti huo
uliofanywa katika nchi za Denmark na Marekani umebaini kuwa wanaume wanaopata
mshahara mdogo, hawashiriki tendo la ndoa kwa ufanisi na wake zao walio na
mishahara mikubwa, ukilinganisha na wanaume walio na kipato kikubwa kuwazidi
wake zao.
Msaidizi
katika utafiti huo Dk Lamar Pierce ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi wa Masuala
ya Mipango katika Chuo Kikuu cha Washington alisema kuwa wanaume huwa dhaifu
kiutendaji katika tendo la ndoa, inapotokea mwanamke ana cheo au kipato kikubwa
kuliko yeye.
Hata hivyo,
utafiti huo haukuwahusisha wanaoishi pamoja bila kufunga ndoa.
Mtafiti huyo
alisema kuwa hali hiyo ni mbaya zaidi katika nchi za Afrika, ambapo mfumodume
umetawala huku mapinduzi ya kijinsia yakianza kushika kasi.
Dk Pierce
alifanya utafiti huo kwa kuchunguza taarifa za sampuli zaidi ya 600,000 za
wakazi wa Denmark, ambapo wanandoa wenye umri wa kuanzia miaka 25 hadi 49
walichunguzwa, kuanzia mwaka 1997 hadi 2006.
Ilibainika
kuwa kwa mabadiliko ya kijamii katika siku za hivi karibuni, wanawake wamekuwa
watafutaji wakuu kuliko wanaume, yamevunja tamaduni na wajibu wa mwanamume,
hali inayowaathiri kisaiokolojia wanaume.
“Hamu ya
tendo la ndoa na ufanisi vinahusiana kwa karibu na kipato, mitandao ya
marafiki, cheo na ile hadhi ya mwanamume kuwa kiongozi katika familia,”
alisema.
Akizungumzia
utafiti huo Dk Kitila Mkumbo, Mhadhiri Mwandamizi katika Saikolojia, Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam alisema kuwa madhara wanayoyapata wanandoa wa aina hiyo
yanasababishwa na tamaduni na mfumodume.
Alisema mila
na desturi zinawafanya wanaume wasijiamini pale wanapochangia kidogo katika
familia.
“Iwapo
mwanamume atamchukulia mke wake kama rafiki na siyo msaidizi wa nyumbani,
hawezi kuathirika, tatizo kubwa ni kuwa wanahisi kukosa hadhi ya ‘ubaba’,”
alisema Mkumbo.
Alisema
kwamba wanaume wengi wa aina hiyo hutoka nje ya ndoa zao kuwatafuta wanawake
wanyonge zaidi yao, ambapo hupata faraja ya tendo la ndoa.
Aliongeza:
“Wanaume wengi, ambao wake zao wana hadhi na kipato kikubwa, mara kwa mara huwa
na hasira, ukali bila sababu, mambo ambayo husababisha waikose raha ya tendo la
ndoa kwa wake zao.”
No comments:
Post a Comment