VIDEO:Jeshi la Polisi Nchini Tanzania lazima maandamano yaliyopangwa na Baadhi ya Waumini wa Kiislamu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumlazimisha Mkurugenzi wa Mashtaka-DPP kuruhusu dhamana ya Shekh Ponda . . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, February 15, 2013

VIDEO:Jeshi la Polisi Nchini Tanzania lazima maandamano yaliyopangwa na Baadhi ya Waumini wa Kiislamu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumlazimisha Mkurugenzi wa Mashtaka-DPP kuruhusu dhamana ya Shekh Ponda . .


Askari wakiwa katika

gari lao wakivinjari

katikakati ya jiji.
Jeshi la Polisi Nchini Tanzania Ijumaa hii limezima(Februari 15,2013) maandamano yaliyopangwa na Baadhi ya Waumini wa Kiislamu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumlazimisha Mkurugenzi wa Mashtaka-DPP kuruhusu dhamana ya Kiongozi wa Kidini.


 

Waandamanaji hao walipigwa marufuku licha ya kuwa waliomba kibali cha kuandamana ili wamuombe DPP atoe idhini ya dhamana kwa kiongozi huyo ambaye ni Katibu wa Shura ya Maimamu na Jumuiya za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda na Wenzake.




Kikosi cha mbwa

hakikuwa nyuma

kuhakisha amani

inakuwepo.
Kaimu Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam, Bw.Ahmed Msangi, alisema pamoja na kuwa jeshi lake halina askari wa kutosha kuwalinda waandamanaji hao lakini pia taarifa zilionyesha kuwa kuna baadhi ya watu wamepanga kufanya vurugu kupitia maandamano hayo.



Waandamanaji hao walipanga kuanza maandamano yao mara tu baada ya kumaliza sala ya Ijumaa katika misikiti mbalimbali ya jijini kuelekea zilipo ofisi hizo.



Taarifa zinasema waandamanji hao wameongeza msukumo wa kudai dhamana ya Sheikh Ponda na wenzake baada ya Elizabeth Michael Msanii wa filamu anayetuhumiwa kumuuwa msanii mwenzake Steven Kanumba kupewa dhamana hivi karibuni.



Sheikh Ponda na wenzake 45 walitiwa nguvuni mwishoni mwa mwaka jana na kesi yao itaendelea kusikilizwa Februari 25 wakikabiliwa na mashitaka manne likiwemo la kuchochea vurugu na uvamizi wa eneo la kampuni moja isivyo halali.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad