Tanzania yaibuka kidedea katika shindano la Maajabu Saba ya Asili ya Afrika kwa kuingiza maajabu matatu,Mlima Kilimanjaro, Mbuga ya Wanyama ya Serengeti na Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, February 12, 2013

Tanzania yaibuka kidedea katika shindano la Maajabu Saba ya Asili ya Afrika kwa kuingiza maajabu matatu,Mlima Kilimanjaro, Mbuga ya Wanyama ya Serengeti na Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.


Tanzania imefanikiwa kushinda kupitia vivutio vyake vitatu vya utalii ambavyo ni Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro Crates na Mbuga ya wanyama ya Serengeti, hafla hiyo imehudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mabalozi,Wafanya biashara,Mawaziri, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na wadau mbalimbali wa utalii kutoka Mataifa mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki.



Maajabu mengine ni Red Sea, Mto Nile ambao zawadi yake ilichukuliwa na Uganda kama asili ya mto huo na Jangwa la Sahara.


Bw Philip Imler Mwanzilishi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders- alitaja wanyama saba wa ajabu Afrika, ambao wote wako Tanzania akiwemo Chui, Tembo, Mamba, Kifaru, Kiboko, Sokwe Mtu na Simba.




Katika  ripoti ya Mkutano wa Uchumi Duniani (WEF) katika vivutio vya utalii, iliitaja Tanzania kuwa ya pili duniani kwa vivutio vizuri baada ya Brazili. 


Sifa ya Kilimanjaro  ilitajwa kuwa Mlima mkubwa wa pekee duniani uliosimama peke yake na wenye theluji wakati uko katika ukanda wa Ikweta wenye joto.


Serengeti ilitajwa kuwa na safari za wanyama aina ya nyumbu ya umbali mkubwa ambayo ni ya pekee ulimwenguni huku Ngorongoro ikitajwa kuwa hifadhi ya pekee duniani yenye mazingira asilia ambayo wanyama pori na binadamu wanaishi pamoja bila kuathiriana.


Mabalozi mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo wa kwanza kutoka kulia ni Balozi Mutinda Mutiso Balozi wa Kenya Nchini Tanzania.


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipiga makofi mara baada ya kumkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi anayenyanyua juu juu tuzo ya Mbuga ya wanyama ya Serengeti mara baada ya kuitangaza mbuga hiyo kuwa ni moja ya maajabu saba ya asili katika bara la Afrika kwenye hoteli ya Mount Meru, Kushoto ni Bw Philip Imler Mwanzilishi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders .


Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Bw. Godbless Lema; kabla ya kuanza kwa hafla hiyo.

Waziri Mkuu akiwa meza kuu pamoja na viongozi wengine wakati wa utoaji wa tuzo hizo za Seven Natural Wonders jijini Arusha jana(Februari 11,2013, kutoka kulia ni Magesa Mulongo mkuu wa Mkoa wa Arusha, Agness Agunyu Waziri wa Utalii kutoka nchini Uganda na kutoka kushoto ni Bw. Philip Imler kutoka Taasisi ya Seven Natural Wonders na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad