Mamia ya Wananchi wakiongozwa na Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein wameungana na waumini wa madhehebu ya kanisa katoliki nchini katika maziko ya padri wa parokia ya St. Joseph ya mjini Zanzibar yaliyofanyika Kitope kaskazini Zanzibar. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, February 20, 2013

Mamia ya Wananchi wakiongozwa na Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein wameungana na waumini wa madhehebu ya kanisa katoliki nchini katika maziko ya padri wa parokia ya St. Joseph ya mjini Zanzibar yaliyofanyika Kitope kaskazini Zanzibar.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein (kushoto) akitoa salamu ya Mwisho kwa mwili wa Marehemu Padri Evarest Mushi, katika Kanisa la Minaramiwili Mjini Zanzibar, Padri Gabriel Mushi, aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikana Jumapili iliyopita, na amezikwa leo (Feb 20,2013)Kijini Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja, katikati ni Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi akiwa na Askofu Augustine Shao askofu wa Jimbo kuu Katoliki Zanzibar wakielekea kwenye mazishiya Marehemu Fr. Evarist Mushi katiI ka  makaburi ya Kitope wilaya ya Kaskazini B Unguja.

Wananchi wa Zanzibar ambao wamehufhuria mazishi ya Fr. Evarist Mushi wakishusha Jeneza lenye mwili wa  Fr. Evarsit Mushi katika Nyumba yake ya Milele  leo katika makaburi ya Kitope wilaya ya Kaskazini B Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi akiweka udongo  katika kaburi la Marehemu Fr. Evaris Mushi katika mazishi yaliyofanyka leo katika makaburi ya Kitope wilaya ya Kaskazini B Unguja.

Waziri wa mambo ya Ndani Mheshimiwa Dr. Emmanuel Nchimbi akiweka udongo katika Kaburi lwa marehemu Fr. Evarist Mushi katika mazishi ambayo yamefanyika leo huko Kitope wilaya ya Kaskazini B Unguja.

Askofu Mkuu  wa jimbo kuu la Dar es salaam Muadhama Policup Pengo pamoja na Maaskofu wengine wakichomeka msalaba katika kaburi la Marehemu Fr. Evarist Mushi katika makaburi ya Kitope wilaya ya Kaskazini B Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi akiweka shada la Maua katika kaburi la Marehemu Fr. Evaris Mushi katika mazishi yaliyofanyka leo katika makaburi ya Kitope wilaya ya Kaskazini B Unguja.







Padri Mushi amezikwa  Zanzibar badala ya kusafirishwa kwenda kwao Moshi mkoani Kilimanjaro, ambapo Askofu Shao: anasema kwamba “Padri Mushi ameishi Zanzibar tangu akiwa na miaka 18 hivyo ni mkazi wa Zanzibar... Hakuna sababu ya kusafirishwa.



Mimi ndiye niliyekuwa mlezi wake hivyo hakuna sababu ya kumpeleka kuzika kwa askofu mwingine.”




Katika Hatua Nyingine , baada ya kuuawa kwa kupigwa risasi Padri Evarist Mushi Mjini Zanzibar, Kanisa la The Pool of Siloam lililoko katika Shehia ya Kianga, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja, limechomwa moto na watu wasiojulikana na kuharibu madhabahu yake.

 

Kuchomwa moto kwa sehemu ya kanisa hilo, kumetonesha kidonda cha kifo cha Padri Mushi ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi kichwani, Jumapili asubuhi mjini Zanzibar. 



Padri huyo amezikwa leo.





Mchungaji Msaidizi wa Kanisa hilo, Penuel Elisha alisema tukio hilo ni la pili kwa kanisa hilo kwani mwaka 2011 zaidi ya watu 80 wakiwa na mapanga, nyundo na magongo walilivamia na kulivunja kabisa.



Alilishukuru Jeshi la Polisi kwa kuwahi kuwasaidia katika tukio la jana.
Licha ya kutotaka kuonyesha uhasama na msikiti uliopo eneo hilo, Penuel alisema siku moja kabla ya tukio hilo viongozi wa msikiti huo walihoji uhalali wa kujengwa kwa kanisa hilo.




Alipoulizwa kuhusu kuwapo kwa uhasama kati ya msikiti na kanisa hilo, Imamu wa msikiti huo, Hassan Migirimu alikanusha akisema kuwa mzozo huo ulikuwa kati ya kanisa na Sheha Assed Mvita ambaye amefariki dunia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad