![]() |
|
Waziri Mkuu wa Tanzania
Mizengo Peter Pinda
|
Waziri Mkuu
Mizengo Pinda ameunda Tume maalum itakayofanya uchunguzi wa matokeo ya mtihani
wa kidato cha nne ambayo yalitangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dokta Shukuru Kawambwa Februari 18, mwaka huu.
Katika
matokeo hayo yaliyotangazwa Jumatatu wiki hii, asilimia 60 ya wanafunzi
waliofanya mtihani wa kidato cha nne Oktoba, 2012 walifeli.
Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu Peniel Lyimo amesema Tume hiyo ambayo inatarajiwa kuanza
kazi wakati wowote wiki ijayo inajumuisha wadau kutoka Chama cha Wamiliki wa
Shule na Vyuo Binafsi (TAMONGSCO), Taasisi za Dini zinazotoa huduma ya elimu,
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs)
zinazoshughulikia masuala ya elimu.
Wadau
wengine watatoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya Bunge ya Huduma za
Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA).
Amesema
Serikali inawaomba wadau wa elimu, wazazi, walezi na wananchi wote kwa ujumla
watoe ushirikiano kwa Tume ili iweze kufanya kazi yake kwa ufanisi.






No comments:
Post a Comment