![]() | |
| Mifugo ya Ng'ombe. |
Mganga
wa mifugo wa wilaya ya Ngara Dr Richard Ngowi amesema hayo kupitia taarifa yake
kwa vyombo ya habari na kwamba Karantini hiyo itaendelea hadi hapo idara yake
itakapojiridhisha kumalizika kwa ugonjwa huo.
Amesema
kuwa hairuhusiwi kusafirisha mifugo kutokana na maeneo mbalimbali ya wilaya ya
Ngara kukabiliwa na ugonjwa wa miguu na midomo ili kukabilina na kuenea zaidi
kwa ugonjwa huo.
Katika
hatua nyingine Halmashauri ya wilaya ya Ngara imeufunga mnada wa mifugo wa
Lumasi ulioko kata ya Kasulo kutokana na ugonjwa huo na kwamba watakaokiuka
agizo hilo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Habari Na:Radio Kwizera FM
Habari Na:Radio Kwizera FM






No comments:
Post a Comment