|
William
Zelothe Stepehen
akiwa
ndani ya ndege
aina
ya Airbus A319.
|
Alipata
mafunzo hayo nchini Uingereza kwa muda wa takriban miezi miwili na amerudi
nchini Tanzania hivi karibuni.
William
alikulia Olosipe jijini Arusha ambapo ni nyumbani kwa wazazi wake.
William
anafananisha anavyojihisi anapoiongoza ndege ya Airbus A319, na wakati akiwa
katika nyumba nzuri ya kifahari na ya kisasa; anaielezea ndege ya Airbus A319
kama ndege iliyo imara na ambayo imewekewa mifumo mingi ya usalama.
|
William
Zelothe Stepehen
akiwa
mbele injini ya ndege
aina
ya Airbus A319punde tu
baada
ya kupokea mafunzo ya
urubani
yaliyodhaminiwa na
shirika la ndege la fastjet
|
Kwa maneno
yake mwenyewe, anasema “Ndege ya Airbus inakulinda kweli kweli, kama unaifahamu
vyema”
William
amewahi kusomea usimamizi wa wanyama pori; alipata mafunzo ya urubani kwa mara
ya kwanza kule Florida Aviation Academy nchini Marekani mwaka 2006 ambapo
alipata leseni yake ya usafirishaji kwa ndege.
Ingawa ana
umri mdogo, ana uzoefu wa masaa 3,053 ya kuongoza ndege.
Kumwajiri
rubani huyu mtanzania mwenye miaka 28, ni mojawapo ya jitihada za fastjet za
kuhakikisha kuwa kampuni hiyo inaajiri watendaji wazawa waliobobea katika fani
hiyo hapa nchini.
William
Zelothe Stepehen
akiwa
ndani ya ndege
aina
ya Airbus A319.
|
Mikakati yao
ya kuajiri pia ni mojawapo ya wajibu wao mpana wa kuwekeza nchini Tanzania.
Kwa
kila rubani aliyepokea mafunzo, fastjet imetumia gharama inayokadiriwa shilingi
49,546,400 hela za kitanzania ambayo ni sawa na 31,027 dola za kimarekani.
fastjet ni
shirika jipya la ndege la nauli nafuu Afrika ambalo lilipata umiliki wa FLY540
na kwa mantiki hiyo likazindua kampuni ya kwanza ya usafiri wa ndege ambalo
linazingatia bajeti.
Fastjet,
ambayo inaungwa mkono na mwanzilishi wa Lonrho na easyGroup Bwana Stelios Haji
Ioannou, imetambulisha nauli za kiwango cha chini hadi kiasi cha Tsh32,000 bila
kujumlisha kodi ili kuwawezesha mamilioni
ya watu ambao walikuwa wameshindwa kusafiri kwa ndege, kuweza kusafiria
ndege kwa mara ya kwanza na kuendelea kutumia ndege mara kwa mara.
Tangu
kuzinduliwa kwake mwezi Novemba 2012, shirika hili la fastjet limewasafirisha
zaidi ya watu 70,000 na asilimia 99.7 ya safari za ndege zikisafiri katika muda
uliopangwa.
Habari Na: kilinyepesiblog





No comments:
Post a Comment