![]() |
|
Wachezaji wa Azam FC
wakimpongeza
Babbi
kufunga bao la kwanza
Katika mchezo huo.
|
Timu ya Azam
FC ya Tanzania imeanza vyema mashindano ya Afrika katika Kombe la
Shirikisho baada ya kuilaza Al Nasir
Juba ya Sudan Kusini mabao 3-1 katika mchezo wa leo Februari 16,2013 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche aliisaidia timu yake ya Azam FC kufunga mabao mawili ndani ya dakika za mwisho na kuipa ushindi timu hiyo.
Kwa matokeo hayo, Azam FC sasa inahitaji sare tu katika mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo nchini Sudan Kusini, au kufungwa si kwa zadi ya tofauti ya bao moja ili kusonga mbele kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Aidha Ligi ya
Mabingwa Afrika inaanza kwa hatua za awali, Tanzania Bara
inayowakilishwa na Simba SC ikianza kazi Jumapili dhidi ya Recreativo de Libolo
ya Angola, wakati wawakilishi wa Zanzibar wakianza na Kedus Giorgis ya Ethiopia
leo, Uwanja wa Gombani, Pemba.






No comments:
Post a Comment