![]() |
| Yanga SC |
Wana
jangwani Yanga SC wameendelea kuwapa raha mashabiki wao baada ya kufanikiwa
kumaliza vema mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kileleni
zaidi kufuatia leo kushinda mabao 2-0
dhidi ya wenyeji Coastal Union Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga katika mchezo wa Ligi kuu VPL.
Yanga
imemaliza mzunguko wa kwanza ikiwa na pointi 29 ikifuatiwa na Azam FC katika nafasi ya pili
yenye pointi 24 na Simba SC nafasi ya tatu kwa pointi zao 23.
Mabao ya Yanga yamefungwa na mshambuliaji wake wa
kimataifa wa Burundi, Didier Kavumbangu na bao la pili, mfungaji akiwa ni Mganda
Hamisi Kiiza .
![]() |
| Simba SC |
Aidha hapo
jana katika Ligi hiyo ya Vodacoma,bao la Dakika ya 73 la mchezaji Musa Saidi Kimbu, liliwapa ushindi ‘Wapwa’
wa Yanga, Toto African wa bao 1-0 dhidi
ya Simba SC katika Mechi ya Ligi Kuu Vodacom VPL, iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na
huko Tanga Mgambo JKT ikawachapa Azam FC bao 2-1 na matokeo hayo yamewabakisha
Yanga kileleni na kuzidisha pengo la uongozi wao.
Simba
walicheza Mechi yao bila Kipa wao Nambari Wani Juma Kaseja ambae amepumzika
baada ya kuletewa kashikashi na Mashabiki wa Simba walipofungwa na Mtibwa Sugar
bao 2-0 katika Mechi yao iliyopita huko Manungu mkoani Morogoro.
![]() |
| Mtibwa Sugar |
Nao Mabingwa
wa Ligi Kuu mwaka 1999 na 2000, Mtibwa
Sugar walilazimika kusawazisha kabla ya kuichapa African Lyon mabao 3-1.
Mshambuliaji
Abdulghan Gulam aliifungia African Lyon bao la kuongoza katika dakika ya 22
akiunganisha kwa kichwa krosi ya Jackson Kanywa.
Mtibwa Sugar
waliamka na kusawazisha bao hilo katika dakika ya 32 kupitia Shabani Nditi
akimalizia pasi ya kinda Hassan Ramadhani, ambapo dakika tatu kabla ya
mapumziko Ally Mohamed alifunga bao la pili kwa Mtibwa akimalizia pasi ya
Hussein Javu.
Kama hiyo
haitoshi, mshambuliaji Javu alifunga bao la tatu kwa Mtibwa akiunganisha vizuri
krosi ya Ally Mohamed katika dakika ya 90.
![]() |
| Tanzania Prisons |
Mkoani Mbeya;
Wenyeji Tanzania Prisons walilazimishwa sare ya 1-1 na JKT Ruvu.
Katika mechi
hiyo mshambuliaji Misango Magae alifunga bao la kuongoza katika dakika ya 10 lakini Jimmy Shoji aliisawazishia JKT Ruvu kwa
shuti kali lililochana nyavu katika dakika ya 87.
Jijini Arusha;
Timu ya Ruvu Shooting ilipata ushindi wao kupitia Seif Rashid aliyefunga mabao
mawili na Michael Pius moja, huku Amiry Omary na Edmund Kashamika wakifunga
mabao mawili ya JKT Oljoro iliyolala kwa mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri
Abeid Arusha.
![]() |
| Kagera Sugar |
Mkoani Kagera;
Kwa upande wa Kagera Sugar wenyewe walilazimishwa sare ya 0-0 na Polisi
Morogoro kwenye Uwanja wa Kaitaba.
RATIBA MECHI
ZIJAZO:
Jumatano
Novemba 14
Mgambo JKT v
Tanzania Prisons [Mkwakwani, Tanga]
Jumapili
Novemba 18
Ruvu
Shooting v Tanzania Prison [Mabatini, Pwani]
RAUNDI YA
PILI YA VPL 2012/2013.
Januari 26
African Lyon
v Simba [National Stadium, Dar es Salaam]
Mtibwa Sugar
v Polisi Morogoro [Manungu, Morogoro]
Coastal
Union v Mgambo JKT [Mkwakwani, Tanga]
Ruvu
Shootings v JKT Ruvu [Mabatini, Pwani]
Azam v
Kagera Sugar [Azam Complex, Dar es Salaam]
JKT Oljoro v
Toto Africans [Sheikh Amri Abeid, Arusha]
Januari 27
Yanga v
Tanzania Prisons [National Stadium, Dar es Salaam]










No comments:
Post a Comment