![]() |
| Real Madrid |
Mabingwa
watetezi wa La Liga Real Madrid jana Novemba 12,mwaka huu kupitia mchezaji wa
timu ya Castilla (Madrid B), Álvaro Morata, kuingia kutokea benchi na kukiokoa
kikosi cha Jose Mourinho kwa kufunga goli la ushindi la dakika za lala salama
dhidi ya Levante jana katika ushindi wa 2-1.
Real Madrid
waliondoka na pointi zote tatu lakini hali ya hewa ilikuwa ngumu katika uwanja
uliojaa maji huku kikosi hicho cha Mourinho kilicheza ovyo lakini Real Madrid walipata goli la kuongoza
katika dakika ya 20 kupitia kwa Cristiano Ronaldo kwa kuwahi mpira wa
'fri-kiki' iliyopigwa na Xabi Alonso na kuukontroo kwa paja lake kabla ya
kufumua shuti lililotinga wavuni.
Goli kutoka
kwa Ángel katika dakika ya 62 liliwafanya wenyeji wapate matumaini ya kupata
pointi na walitishia kuizamisha timu ya Mourinho na Xavi Alonso alipoteza
nafasi muhimu wakati penalti yake aliyopiga kupanguliwa na kipa wa Uruguay Munúa.
![]() |
| Messi na Alexis |
Aidha nyota
wa FC Barcelona Lionel Messi amevunja
rekodi iliyowekwa na gwiji wa Brazil
Pele baada ya kufunga magoli
mawili yaliyoisaidia timu yake kushinda 4-2 ugenini juzi dhidi ya Real Mallorca
.
Messi sasa
amefikisha magoli 76 katika mwaka 2012, moja zaidi ya rekodi iliyowekwa na Pele
mwaka 1958 ya magoli 75.
Pele aliweka
rekodi hiyo katika mechi 53 alizoichezea klabu yake ya Santos na timu ya taifa
ya Brazil wakati Messi ametumia mechi 59
alizoichezea klabu yake ya FC Barcelona na timu yake ya taifa ya Argentina.
Messi sasa
amebakisha magoli 9 kufikia rekodi ya wakati wote iliyowekwa na gwiji wa
Ujerumani Gerd Muller ambaye alifunga
magoli 85 katika msimu wa mwaka 1972 rekodi ambayo haipewi nafasi sana kwa
sababu magoli 12 kati ya hayo 85, aliyafunga katika michuano ya Football League
Cup, ambayo haikuwa michuano rasmi wakati huo.
Barcelona
pia imefikia rekodi ya La Liga ya kuwa na mwanzo mzuri zaidi wa msimu kutokana
na kushinda mechi 10 na sare moja rekodi
iliyokuwa ikishikiliwa na Real Madrid katika misimu miwili ya 1968-69 na 1991-92.
La Liga Msimamo:
1 FC Barcelona Pointi 31
2 Atletico Madrid 28
3 Real Madrid 23
4 Real Betis 19
5 Malaga 18
6 Levante 17
Matokeo:
Rayo Vallecano 3 v 2 Celta Vigo
Espanyol 0 v 3 Osasuna
Real Zaragoza 5 v 3 Deportivo La Coruna
Malaga 1 v 2 Real Sociedad
Real Valladolid 1 v 1 Valencia
Athletic Bilbao 2 v 1 Swvilla
Real Mallorca 2 v 4 Barcelona
Atletico Madrid 2 v 0 Getafa
Levante 1 v 2 Real Madrid
![]() |
| Manchester City |
Msimamo:
1 Man United Mechi
11 Pointi 27
2 Man City
Mechi 11 Pointi 25
3 Chelsea Mechi 11
Pointi 24
4 Everton Mechi 11
Pointi 20
5 WBA Mechi 11
Pointi 20
6 West Ham Mechi
11 Pointi 18
7 Tottenham Mechi
11 17
8 Arsenal Mechi 11
Pointi 16
Matokeo:
Arsenal 3 v 3
Fulham
Everton 2 v 1 Sunderland
Reading 0 v 0
Norwich City
Southampton 1 v 1 Swansea
City
Stoke City 1 v 0
Queens Park Rangers
Wigan Athletic 1 v
2 West Brom
Aston Villa 2 v 3
Manchester United
![]() |
| Juventus |
Matokeo:
Cagliari 0 v 0 Catania
Pescara 1 v 6 Juventus
Palermo 2 v 0 Sampdoria
Genoa 2 v 4 Napoli
Chievo Verona 2 v 2 Udinese
AC Milan 1 v 3 Fiorentina
Torino 1 v 0 Bologna
Parma 0 v 0 Siena
Lazio 3 v 2 AS Roma
Atalanta 3 v 2 Inter Milan
Msimamo:
1 Juventus Pointi 31
2 Inter Milan 27
3 Napoli 26
4 Fiorentina 24
5 Lazio 22
![]() |
| Bayern Munich |
BUNDESLIGA:
Matokeo:
Freiburg 0 v 0 Hamburger
Schalke 2 v 1 Werder Bremen
Bayern Munich 2 v 0 Eintracht Frankfurt
Augsburg 1 v 3 Borussia Dortmund
Fortuna Dusseldorf 1 v 1 Hoffenheim
Wolfsburg 3 v 1 Bayer Leverkusen
SpVgg Gr. Furth 2 v 4 Borussia Monchengladbach
Stuttgart 2 v 4 Hannover
Msimamo:
1 Bayern Munich Pointi 30
2 Schalke 23
3 Eintracht Frankfurt 20
4 Borussia Dortmund 19
5 Bayer Leverkusen 18
6 Hannover 17










No comments:
Post a Comment