![]() |
|
Mwenyekiti
wa CCM
Rais Jakaya Kikwete
|
Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kimeunda Sekretarieti
mpya katika uongozi wake huku wakongwe
wakirejeshwa akiwamo Abdulrahaman Kinana
aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho.
Kinana
mwanasiasa wa siku nyingi ambaye amekitumikia chama hicho kwa miaka 25,
anachukua nafasi ya mtangulizi wake, Wilson Mukama ambaye ameng’olewa katika
nafasi hiyo na kuweka rekodi ya kuwa Katibu Mkuu aliyekaa kwa muda mfupi wa
miaka miwili tu.
Wengine
katika Sekretarieti iliyotangazwa jana na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya
Kikwete ni pamoja na Mbunge wa Kuteuliwa, Zakhia Meghji, Mbunge wa Uzini,
Mohamed Seif Khatibu na Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Dk Asha-
Rose Migiro.
![]() |
|
Abdulrahman
Kinana
Katibu
Mkuu wa CCM, Taifa
|
Akitangaza
safu hiyo mpya ya uongozi baada ya kumalizika kikao cha Halmashauri Kuu (Nec) ya chama hicho
kilichofanyika katika Ukumbi wa White House jana, Rais Kikwete aliwataja
wengine aliowateua kuwa ni Vuai Ali Vuai ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.
Alisema
Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba amepandishwa kutoka Katibu Uchumi
na Fedha na kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara, akichukua nafasi iliyokuwa
ikishikiliwa na Mbunge wa Manyoni Mashariki, John Chiligati.
![]() |
|
Mwigulu
Nchemba
Naibu
Katibu Mkuu (Bara)
|
Alisema
Meghji atakuwa Katibu wa Uchumi na Fedha
akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Nchemba, wakati Khatib ameteuliwa
kuwa katibu wa Oganaizesheni ya chama hicho, nafasi ambayo katika Sekretarieti
iliyopita ilikuwa ikishikiliwa na Asha Abdallah Juma.
Dk
Migiro ameteuliwa kuwa Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, nafasi ambayo
ilikuwa ikishikiliwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
January Makamba.
Kwa
mujibu wa kanuni za CCM, mawaziri hawaruhusiwi kuwa watendaji katika
sekretarieti ya chama, hivyo Makamba asingeweza kuteuliwa tena isipokuwa kwa
sababu maalumu.
Dk
Migiro kama ilivyo kwa Meghji aliwahi kushika wadhifa huo kabla ya kuteuliwa
kwenda Umoja wa Mataifa.
Rais Kikwete alisema chama hicho kimemteua Nape Nnauye
kuendelea na wadhifa wake wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama.
![]() |
|
Vuai
Ali Vuai
Naibu
Katibu Mkuu (Zanzibar)
|
Alisema
ameshindwa kuteua wajumbe wa Kamati Kuu kwa sababu wajumbe wa Nec bado ni wapya
na kwamba apewe muda wa kuangalia atakaowateua.
“Uteuzi
wa Kamati Kuu, utafanyika baadaye kwa sababu Nec hii ina watu wazuri na wapya,
hivyo nipeni muda niangalie nani nimteue kuingia katika Kamati Kuu,” alisema.
Walioachwa.
Mukama
aliyechukua nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM 2010, amepewa jukumu la kusimamia
uanzishwaji wa chuo cha chama hicho.
Katika
uongozi wake, kiongozi huyo amekuwa akilalamikiwa na makada wa CCM ambao
wamekuwa hawaridhishwi na utendaji wake tangu alipoteuliwa, hasa kuhusu
utekelezaji wa mpango wa kujivua gamba ambao ulilenga kuwang’oa watuhumiwa wa
ufisadi.
Alitikiswa
na siasa za makundi ambayo yamekuwa yakipata nguvu kila kukicha, kutokana na
kujipanga kuwania urais wa 2015 kupitia CCM, na katika Uchaguzi Mkuu wa chama
hicho, alionekana kushindwa kukimudu chama kutokana na kushamiri kwa rushwa.
![]() |
|
Nape
Nnauye
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi
|
Mukama
akizungumzia uteuzi wa kuongoza uanzishwaji wa chuo cha CCM alisema amefurahi
kufanya kazi hiyo.
Alisema:
“Nimefurahi sana, sina wasiwasi na majukumu mapya ambayo nimepewa, nitayamudu.”
Chiligati
kwa upande wake anaondoka katika chama hicho baada ya kudumu kwa muda mrefu akiwa
mjumbe wa Sekretarieti.
Awali
alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi na baadaye alipandishwa wadhifa na kuwa
Naibu Katibu Mkuu (Bara), nafasi iliyompa misukosuko hasa katika kipindi
ambacho CCM kilijaribu kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi.
Kwa
upande wake, Asha Abdallah Juma, yeye ameachwa kutokana na umri, hali ambayo
imekuwa ikimfanya ashindwe kushiriki kikamilifu katika harakati za kisiasa
ndani ya CCM.
![]() |
|
Asha-Rose
Migiro
Katibu wa NEC,
Siasa
na Uhusiano wa Kimataifa
|
Kada
huyo wakati wa uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki mwezi Aprili mwaka huu,
alikuwa akitembelea fimbo na hakuwa na uwezo wa kusimama jukwaani kwa muda
mrefu.
Kikosi
cha 2015.
Makada
wapya walioteuliwa wanaungana na mkongwe mwingine, Makamu Mwenyekiti Bara,
Phillip Mangula aliyerejeshwa katika uongozi wa juu wa chama, baada ya kuwa nje
kwa miaka mingi.
Mangula
aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM wakati wa uongozi wa Benjamin Mkapa alipata nafasi
hiyo baada ya kukosa nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Iringa
katika uchaguzi uliopita. Baada ya kukosa nafasi hiyo aliendelea na shughuli za
kilimo mkoani humo.
Mangula
kama alivyo Kinana wanatajwa kuwa watu makini na kuwepo kwao katika nafasi za
juu za uongozi wa CCM ni ishara kwamba huenda chama hicho kimeamua kujipanga
ipasavyo kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Mangula
ni mmoja wa makada wa CCM walioitwa kuokoa jahazi la chama hicho lisizame
katika uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Igunga, ambako anatajwa kuwa
alisaidia kuwabaini hata makada ambao walikuwa wakitoa taarifa za uongo kuhusu
uchaguzi huo.
![]() |
|
Zakhia Meghji
Katibu
wa NEC, Uchumi na Fedha
|
Kinana
kama alivyo Mangula, amejizolea sifa ya kuwa kiongozi mkuu wa kampeni za CCM
tangu kuanza kwa siasa za vyama vingi nchini 1995, na tangu wakati huo chama
hicho hakijawahi kushindwa.
Siku
chache zilizopita alitangaza rasmi kustaafu siasa ndani ya CCM, hatua ambayo
iliwashtua sana makada wa chama hicho wakiwamo vigogo ambao tayari walikuwa
wameanza kumshawishi kukubali uteuzi wa nafasi ya Katibu Mkuu.
Habari
kutoka ndani ya CCM zinasema, kulikuwa na kazi kubwa ya kumshawishi kukubali
wadhifa huo na kwamba alitoa masharti magumu ambayo vigogo wa chama hicho
walilazimika kuyakubali ili “kukinusuru chama”.
Kauli
za wateule.
Akizungumzia
kuteuliwa kwake, Kinana alisema ameupokea kwa furaha uteuzi huo ingawa ni
dhamana nzito kuibeba.
Hata
hivyo, alisema atajitahidi kadiri ya uwezo wake kumsaidia Mwenyekiti wa chama
hicho kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM.
Kinana
alisema ingawa hivi karibuni alitangaza kustaafu uongozi ndani ya chama hicho,
lakini aliombwa na Rais Kikwete amsaidie, hivyo asingeweza kukataa.
Alisema
uamuzi wa kustaafu uongozi ulikuwa uamuzi wake binafsi baada ya kukaa katika
uongozi wa chama kwa miaka 25.
![]() |
|
Muhamed
Seif Khatib,
Katibu
wa NEC, Oganaizesheni
|
Kinana
alisema aliona ni vyema kukaa pembeni ili watu wengine ndani ya chama hivyo
hususan vijana kuchukua nafasi za uongozi.
Kuhusu
uadilifu ndani ya chama hicho, alisema atatekeleza uamuzi wote wa vikao na
kwamba watautengenezea programu ya utekelezaji wake.
Kwa
upande wake, Meghji alisema amefurahi kuteuliwa katika nafasi hiyo ambayo
inamwezesha kukitumikia chama tena.
Alisema
nafasi ya Katibu wa Uchumi na Fedha wa chama ina changamoto nyingi hasa kwa
wakati huu ambapo chama hicho, kimeamua kujitegemea kiuchumi.
Hata
hivyo, alisema anaamini kuwa atashirikiana na viongozi na wanachama wengine ili
kufanikiwa kwa mipango hiyo ya chama.
“Naamini
kuwa tutafanikiwa kufikia lengo hilo la chama kwa sababu tutashirikiana wote,”
alisema.
Naye
Dk Migiro alisema ameupokea uteuzi huo kwa furaha, kwa sababu ni kazi ya
kukijenga chama chao.
Alisema
kwake yeye ni heshima kubwa kupewa majukumu hayo ya kuitumikia nchi yake
kupitia CCM.
“Ni
heshima kubwa kupewa majukumu haya ya kuitumikia nchi yangu,” alisema.
Naye
Mwingulu alisema ameufurahia uteuzi huo kwa sababu hakutarajia kuwa katika timu
hiyo mpya.
Alisema amefurahishwa kupangwa katika timu mpya ya
uongozi wa chama hicho ambayo anaamini ni ya ushindi.
“Nimepokea
uteuzi, kwa mshtuko mkubwa na furaha , nimefurahishwa na timu mpya ambayo nimo
ndani yake,” alisema.
Habari na:
http://www.mwananchi.co.tz













No comments:
Post a Comment