Cheki matokeo ya Ligi za Ulaya, Lionel Messi wa FC Barcelona akivunja rekodi ya Pele wakati Juventus na Bayern wakipata ushindi huku Chelsea ikishuka katika msimamo wa Ligi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, November 12, 2012

Cheki matokeo ya Ligi za Ulaya, Lionel Messi wa FC Barcelona akivunja rekodi ya Pele wakati Juventus na Bayern wakipata ushindi huku Chelsea ikishuka katika msimamo wa Ligi.

Real Madrid
Mabingwa watetezi wa La Liga  Real Madrid  jana Novemba 12,mwaka huu kupitia mchezaji wa timu ya Castilla (Madrid B), Álvaro Morata, kuingia kutokea benchi na kukiokoa kikosi cha Jose Mourinho kwa kufunga goli la ushindi la dakika za lala salama dhidi ya Levante jana katika ushindi wa 2-1.




Real Madrid waliondoka na pointi zote tatu lakini hali ya hewa ilikuwa ngumu katika uwanja uliojaa maji huku kikosi hicho cha Mourinho kilicheza ovyo  lakini Real Madrid walipata goli la kuongoza katika dakika ya 20 kupitia kwa Cristiano Ronaldo kwa kuwahi mpira wa 'fri-kiki' iliyopigwa na Xabi Alonso na kuukontroo kwa paja lake kabla ya kufumua shuti lililotinga wavuni.


Goli kutoka kwa Ángel katika dakika ya 62 liliwafanya wenyeji wapate matumaini ya kupata pointi na walitishia kuizamisha timu ya Mourinho na Xavi Alonso alipoteza nafasi muhimu wakati penalti yake aliyopiga kupanguliwa na kipa wa Uruguay  Munúa.



Messi na Alexis
Aidha nyota wa FC Barcelona Lionel Messi  amevunja rekodi iliyowekwa na gwiji wa Brazil  Pele  baada ya kufunga magoli mawili yaliyoisaidia timu yake kushinda 4-2 ugenini juzi dhidi ya Real Mallorca .



Messi sasa amefikisha magoli 76 katika mwaka 2012, moja zaidi ya rekodi iliyowekwa na Pele mwaka 1958 ya magoli 75.


Pele aliweka rekodi hiyo katika mechi 53 alizoichezea klabu yake ya Santos na timu ya taifa ya Brazil  wakati Messi ametumia mechi 59 alizoichezea klabu yake ya FC Barcelona na timu yake ya taifa ya Argentina.


Messi sasa amebakisha magoli 9 kufikia rekodi ya wakati wote iliyowekwa na gwiji wa Ujerumani  Gerd Muller ambaye alifunga magoli 85 katika msimu wa mwaka 1972 rekodi ambayo haipewi nafasi sana kwa sababu magoli 12 kati ya hayo 85, aliyafunga katika michuano ya Football League Cup, ambayo haikuwa michuano rasmi wakati huo.


Barcelona pia imefikia rekodi ya La Liga ya kuwa na mwanzo mzuri zaidi wa msimu kutokana na kushinda mechi 10 na sare moja  rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Real Madrid katika misimu miwili ya 1968-69 na 1991-92.



La Liga  Msimamo:


1 FC Barcelona Pointi 31

2 Atletico Madrid  28

3 Real Madrid  23

4 Real Betis  19

5 Malaga  18

6 Levante  17


Matokeo:


Rayo Vallecano 3 v 2 Celta Vigo 

Espanyol 0 v 3  Osasuna 

Real Zaragoza 5 v 3 Deportivo La Coruna 

Malaga 1 v 2  Real Sociedad 

Real Valladolid 1 v 1  Valencia 

Athletic Bilbao 2 v 1  Swvilla 

Real Mallorca 2 v 4  Barcelona 

Atletico Madrid 2 v 0 Getafa 

Levante 1 v 2  Real Madrid 



Manchester City
Huko nchini Uingereza ,Nahodha John Terry akiichezea Mechi yake ya kwanza ya Ligi tangu afungiwe Mechi 4 aliifungia Chelsea bao moja lakini Liverpool walizinduka na kusawazisha kupitia Luis Suarez na Mechi kumalizika 1-1 na kuwafanya Chelsea waipishe Manchester City kwenye nafasi ya pili wakiwa nyuma ya vinara Manchester United.



Mchezaji Eden Dzeko aliwapa ushindi Mabingwa watetezi Manchester City kwa kufunga bao la pili na la ushindi katika Dakika ya 88 walipoifunga Tottenham bao 2-1 baada ya kutanguliwa bao lilifungwa na Caulker na Aguero akaisawazishia City.


Msimamo:


1 Man United Mechi 11 Pointi 27

2 Man City  Mechi 11 Pointi 25

3 Chelsea Mechi 11 Pointi 24

4 Everton Mechi 11 Pointi 20

5 WBA Mechi 11 Pointi 20

6 West Ham Mechi 11 Pointi 18

7 Tottenham Mechi 11 17

8 Arsenal Mechi 11 Pointi 16



Matokeo:


Arsenal 3 v 3 Fulham

Everton 2 v 1  Sunderland 

Reading 0 v 0 Norwich City 

Southampton 1 v 1 Swansea City 

Stoke City 1 v 0 Queens Park Rangers 

Wigan Athletic 1 v 2 West Brom

Aston Villa 2 v 3 Manchester United 



 Juventus
Katika Ligi ya  Serie A,nchini Italia  Juventus iliifumua Pescara bao 6-1 na kuzidi kujiimarisha kileleni mwa ligi hiyo.


SERIE A:


Matokeo:

Cagliari 0 v 0 Catania 

Pescara 1 v 6 Juventus 

Palermo 2 v 0 Sampdoria 

Genoa 2 v 4  Napoli 

Chievo Verona 2 v 2 Udinese 

AC Milan 1 v 3 Fiorentina 

Torino 1 v 0  Bologna 

Parma 0 v 0 Siena 

Lazio 3 v 2  AS Roma 

Atalanta 3 v 2 Inter Milan 


Msimamo:


1 Juventus Pointi 31

2 Inter Milan 27

3 Napoli 26

4 Fiorentina 24

5 Lazio 22



Bayern Munich
Nako kwenye Bundesliga,Ligi kuu soka Ujerumani ,Timu ya  Bayern Munich iliichapa Eintracht Frankfurt 2-0 na kuzidisha pengo la point 7 dhidi ya Schalke 04 wanaowafatia katika msimamo.




BUNDESLIGA:


Matokeo:


Freiburg 0 v 0 Hamburger 

Schalke 2 v 1  Werder Bremen 

Bayern Munich 2 v 0 Eintracht Frankfurt 

Augsburg 1 v 3 Borussia Dortmund 

Fortuna Dusseldorf 1 v 1 Hoffenheim 

Wolfsburg 3 v 1 Bayer Leverkusen 

SpVgg Gr. Furth 2 v 4 Borussia Monchengladbach 

Stuttgart 2 v 4 Hannover 


Msimamo:


1 Bayern Munich Pointi 30

2 Schalke 23

3 Eintracht Frankfurt 20

4 Borussia Dortmund 19

5 Bayer Leverkusen 18

6 Hannover 17



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad