Real Madrid wameitandika FC Barcelona ndani ya dimba la Santiago Bernabeu na kubeba Ubingwa SUPERCUP 2012/2013 huku Messi akivunja rekodi ya Cesar Rodriguez na Ronaldo akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa pili kufunga mara 5 mfululizo kwenye mechi ya 'EL CLASICO!' - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, August 30, 2012

Real Madrid wameitandika FC Barcelona ndani ya dimba la Santiago Bernabeu na kubeba Ubingwa SUPERCUP 2012/2013 huku Messi akivunja rekodi ya Cesar Rodriguez na Ronaldo akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa pili kufunga mara 5 mfululizo kwenye mechi ya 'EL CLASICO!'

We are the champions, super copa de espana!''Halla aaaa Madrid


Luka Modric wa Croatia alienunuliwa kutoka Tottenham akionekana Uwanjani.


Katika hali ya kawaida hasa Siku hizi, huwezi kuitaja Real Madrid au FC Barcelona bila ya kuwataja Wachezaji wanaosifika Duniani, Cristiano Ronaldo wa Real na Lionel Messi  kwani hawa wawili wamewika kwenye Mechi ya aina hii kubwa jina maalum, 'EL CLASICO!'


Dk 19′ Cristiano Ronaldo


Aidha Jose Mourinho alikiongoza kikosi chake cha Real Madrid kuwafunga mahasimu wao wakubwa FC Barcelona bao 2-1 kwenye mchezo wa pili wa kogembea kombe la Supercup kwenye uwanja wa Santiago Bernebeu. Kwa matokeo hayo timu hizo zikafunga kwa jumla ya mabao 4-4, lakini kutoka na Madrid kuwa na idadi kubwa ya magoli ya ugenini wakatwaa ubingwa huo wa tatu tangu Mourinho afike Bernebeu.



Dk 11′ Gonzalo Higuaín



Kwa maana hiyo baada ya kufanikiwa kutwaa uchampion huo wa Supercup, Mourinho anaweka historia nyingine kubwa duniani akiwa ndio kocha pekee kuwahi kutwaa makombe ya ligi na supercup - (ambalo hukutanisha bingwa wa ligi na bingwa wa kombe la FA ya nchi husika -au mshindi wa pili wa ligi) katika nchi nne tofauti zilizo juu kwenye viwango vya FIFA - Uingereza alichukua EPL na Community shield, Ureno walifanya hivyo hivyo, Italia pia na sasa Hispania.




Its a great feeling winning the Supercopa with our supporters. Thank you. Hala Madrid!


Real Madrid - FC Barcelona: Super Cup slips away (2-1)



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad