|
Jengo la Afya Kituo cha Afya Murusagamba.
Naye Kaimu
Mganga mkuu wa wilaya ya Ngara Dkt
Godian Beyanga alisema upanuzi wa kituo cha Afya Murusagamba kinakadiriwa
kuhudumia watu 36,060 katika vijiji tisa na vitongoji 53 kata za
Murusagamba, Muganza na Nyamagoma na kitasaidia wananchi wanaotumia gharama
kubwa hadi Hospitali ya wilaya hiyo.
“Upanuzi wa kituo hiki bado unahitaji umeme wa
uhakika kihuduma maana unaotumika ni wakutegemea jua jambo ambalo ni hatari
wakati wa mvua kufanya upasuaji kwa wanawake wajawazito wanaojifungua” Alisema
Dkt Beyanga.
Hata hivyo
Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo Bw.Ghalib Mkumbwa alisema kituo cha Afya cha kata ya Bukiriro kinachotegemewa na kata saba kinasubiria fedha toka Serikalini
kupanua majengo yake kuhudumia wananchi kwa sekta ya Afya .
|
|
Mazungumzo na Watumishi wa Kituo cha Afya Mabawe.
Akiwa kituo
cha Afya Mabawe, Mhe.Nkilamachumu
aliwataka wajumbe wa kamati ya ujenzi kuacha malumbano ya kusimamia majengo
yaliyoanzishwa,bali wafanye vikao vya
maamuzi na kushirikisha wananchi kusogeza vifaa vinavyohitajika.
Kituo cha
Afya Mabawe kinahudumia wakazi 15,654 kutoka vijiji vitano vya kata ya
Mabawe na vingine vya kata ya Kabanga, Kanazi na Mugoma ambapo wananchi
hufika kupewa huduma za matibabu kwa maradhi ya aina mbalimbali.
Aidha
aliwashauri wananchi kuchangia bima ya Afya kupitia CHF Sh15,000 kila kaya na kutibiwa
watu sita mwaka mzima, na kuagiza uongozi wa kituo hicho kupunguza gharama za
kulaza wagonjwa kutoka Sh10,000 kwa siku hadi Sh2,000.
|
Jengo katika kituo cha afya Mabawe.
Picha/Habari Na
Shaaban Ndyamukama.
|





No comments:
Post a Comment