![]() |
|
Eneo la Kuchezea katika Uwanja huo wa Kokoto.
Ikumbukwe
kuwa , Viwanja vya soka
ni mahali pa hisia za kimichezo na mvuto kwa watu wengi. Ni sehemu ambayo
hutumiwa na maelfu ya watu bila kujali tofauti za itikadi zao za kisiasa,
kidini, kijamii na jinsia, kuburudishwa na mechi za mpira wa miguu.
Katika miaka
ya karibuni, kumekuwa na kukua kwa kiwango cha soka wilayani Ngara ambako
kimekwenda sambamba na ongezeko la wapenzi na watazamaji wa mchezo huo na kupata mafanikio ya Timu za Murusagamba FC kuwa Mabingwa wa Mkoa wa Kagera 2015/2016 na Mabingwa wa sasa Kumuyange FC 2017/2018 huku Timu zake za soka zikinyanyasa vilivyo timu zingine za mkoa wa Kagera.
Hata hivyo, ongezeko hilo haliendi sanjari na ujenzi wa kiwanja hicho cha Kokoto au viwanja vipya pamoja na upanuzi na uboreshaji wa kuridhisha wa vile vilivyopo vya Kemikimba kilichopo mjini Benaco, Ule wa Kabanga uliopo Mjini Kabanga na ule wa Nazareth mjini Rulenge. |
![]() |
|
Rulenge
Stars Mabingwa wa Polisi Jamii Cup 2018/2019 licha ya kupata ugumu katika
uchezaji sababu ya ubora wa uwanja wa Kokoto lakini Timu huwa zinapambana
kuonesha soka safi ili kupata matokeo mazuri dhidi ya wapinzani wao.
Aidha,
Aprili 22 wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha
za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2016/2017, Majaliwa alisema serikali
itaendelea kuimarisha michezo nchini ili kuwawezesha wanamichezo kufanya vizuri
kitaifa na kimataifa.
“Kutokana na
umuhimu wa michezo katika kuimarisha afya, kuongeza ajira, kujenga udugu na
mshikamano miongoni mwa jamii na mataifa mbalimbali duniani, serikali
itaendelea kuimarisha sekta hiyo kwa kusimamia maendeleo ya michezo katika
shule, vyuo, taasisi na vilabu,” alisema kiongozi huyo wa serikali.
Majaliwa
ambaye alitoa ahadi hiyo, ni kocha mwenye Leseni B ya Shirikisho la Soka Afrika
(Caf).
|
![]() |
|
Uchunguzi
umebaini pia uwanja huu kutotoa fursa kwa Watazamaji kukaa kwa raha na starehe wakati wa mechi
pamoja na kukosa uzio madhubuti wa kuzuia watazamaji kuwafikia wachezaji na waamuzi.
Je
Halmashauri ya wilaya ya Ngara mnaufikiriaje uwanja huu wa Kokoto?? Ikiwa Serikali
ya Awamu ya Tano ikiahidi kuinua michezo nchini??
|










No comments:
Post a Comment