NA BASHIR YAKUB -
Kumekuwepo na
sintofahamu nyingi kwa madereva na
watumiaji wengine wa vyombo vya usafiri.
Sintofahamu hii imekuwa ikiletwa na
baadhi ya mambo ambayo hayaeleweki sawasawa
katika suala zima la usalama
barabarani na sheria zake.
Wadau wa
barabarani wamekuwa wakilaumiana, madereva wakiwalaumu
askari wa barabarani kwa uonevu huku askari
wa barabarani wakiwalaumu madereva kwa
ukorofi na ukosefu wa utii wa sheria
bila shuruti.
Lakini swali hapa ni kwanini
iwepo mivutano na hali kuna sheria. Sheria
inasemaje kwa kila jambo ambalo wadau
hawa wanatofautiana?.
1.UBABE WA ASKARI
WA BARABARANI.
Baadhi ya askari
wa barabarani wamekuwa ni wababe sana.
Wanahoji mambo ambayo si wajibu wao
kuyahoji na hawataki dereva aulize lolote
kuhusu kuhoji kwao mambo hayo.
Wanataka
kila wanachosema dereva atii hata kama anaona
hakipo kwa mujibu wa sheria. Matokeo yake
mtu anaandikiwa faini za makosa mengi
ilimradi tu kumkomoa. Askari wengine wamefikia
hatua ya kuwapiga madereva vibao.
Binafsi
nimewahi kushuhudia askari wa usalama
barabarani akimnasa kibao dereva wa daladala. Ni
ubabe uliovuka mipaka na hakika ni
uvunjaji wa sheria uliopitiliza .
2. JE TRAFIKI
ANARUHUSIWA KUMNYANGANYA DEREVA LESENI.
Masuala ya usalama
barabarani yanaainishwa ndani ya Sheria
ya Usalama barabarani ( The Road Traffic Act) ambayo
ndio hueleza wajibu na haki za
kila mdau na mtumiaji wa barabara.
Katika
sheria hii hakuna pahala pameandikwa kuwa
trafiki achukue leseni ya dereva kwa
kuwa dereva ametenda kosa fulani.
Maana
fupi ya hili ni kuwa trafiki haruhusiwi
kuchukua leseni ya dereva. Anachoweza kufanya
trafiki ni kile kilichoainishwa na kifungu
cha 17 cha sheria hiyo ya usalama
barabarani.
Kifungu hicho kinampa trafiki mamlaka
ya kukagua na kujiridhisha na uhalali
wa leseni ya dereva. Hakisemi aichukue. Kinasema
aikague basi. Kukagua na kuchukua ni
mambo mawili tofauti.
Kama hivyo ndivyo
basi yafaa kueleweka kuwa kitendo cha
askari kumsimamisha dereva na kisha
kumpokonya leseni yake ni kinyume cha
sheria.
Dereva anao wajibu
wa kulinda haki hii kwa kulikataa
hili na kuhakikisha trafiki hamfanyii kitendo hiki.
Kumbuka kuwa wakati askari wa barabarani
akitekeleza wajibu wake wa kisheria na wewe
dereva unayo haki ya kutetea haki
zako za kisheria. Hakuna aliye juu ya
mwingine kwani anatekeleza wajibu nawe unalinda
haki.
3. SAID
MWEMA AKATAZA KUNYANGANYWA LESENI.
Mkuu wa
jeshi la polisi mstaafu ndugu Saidi Mwema
aliwahi kuandika kukemea hatua ya madereva
kunyanganywa leseni. Katika kijarida alichokiita
UMESIMAMISHWA NA POLISI UKIWA UNAENDESHA ?, ZIJUE
HAKI NA WAJIBU WAKO, ndugu mwema
ameandika akisema kuwa ofisa wa
polisi hana haki ya kuchukua leseni
ya dereva.
4. HAIRUHUSIWI KUBANDUA
BIMA/ AU KIBANDIKO( STICKERS) KINGINE CHOCHOTE.
Wakati mwingine
askari wa barabarani huamua kubandua bima
au vibandiko vingine ( stickers) kwa lengo la
kumfanya dereva amfuate au malengo mengine
yoyote.
Hili nalo ni kosa kwakuwa
haliainishwi popote katika sheria. Jambo
ambalo halikuruhusiwa na sheria kulitenda
kwake ni kosa. Ieleweke kuwa askari wa
barabarani haruhusiwi kubandua stika yoyote
katika gari lako wala kuichukua.
5. UKIONEWA NA
ASKARI WA BARABARANI CHUKUA HATUA HIZI.
Ili uweze
kumchukulia hatua vizuri askari ni
vema ukijua jina lake, cheo chake, na kituo
anachotokea.
Katika kuyajua haya ni lazima watu
wajue kuwa ni haki yako kumuuliza askari
taarifa hizi. Sio dhambi wala kosa
ila ni haki kumuuliza askari taarifa
hizi. Na kwa askari ni wajibu
kukueleza taarifa hizi.
Haijalishi mmeshatofautiana
wala nini isipokuwa ni wajibu akupe
taarifa hizi. Lakini ushauri ni kuwa ni
vema zaidi askari anapokusimamisha tu kabla
ya kujadili lolote kumuuliza au kumuomba ajitambulishe
ili hata mkishatofautiana mbeleni iwe rahisi
kwako kuchukua hatua.
Kiutaratibu inatakiwa
askari ajitambulishe kwako bila wewe kumuuliza na
kabla ya kuzungumza lolote lakini kwakuwa
hawafanyi hivyo ndio maana wewe unalazimika
kumuuliza. Baada ya kupata taarifa hizo
peleka malalamiko yako kwa mkuu wa
kituo anachotokea halafu fuatilia.
Atachukuliwa
hatua wala huna haja ya kulihofi hilo.
Jeshi la polisi ni sehemu ambako nidhamu
inazingatiwa kuliko pahali pengine popote
hivyo unapomripoti askari ni lazima
ashughulikiwe.
Kwa taarifa yako askari
wanaogopa sana kuripotiwa kwa wakubwa zao kuliko
watumishi wengine wowote wa umma unaowajua, hili
nakupa. Na askari yoyote mwenye kujitambua
akijua unalenga kumripoti ni lazima akubali
myamalize.
Basi usiishie kulalamika kwani kulalamika
hakusaidii chukua hatua ili iwe funzo
kwa wengine kesho na mbeleni.....BOFYA
HAPA KUSOMA ZAIDI
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI MWANASHERIA NA
MSHAURI WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA
SERIKALI LA HABARI LEO KILA
JUMANNE , GAZETI JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE KILA JUMATANO.
0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
|
Thursday, August 13, 2015
Home
HABARI
SHERIA YETU:-Je Askari wa Usalama Barabarani ( TRAFIKI ) anaruhusiwa Kukunyang’anya Leseni.??
SHERIA YETU:-Je Askari wa Usalama Barabarani ( TRAFIKI ) anaruhusiwa Kukunyang’anya Leseni.??
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment