![]() |
Jenni Furuguti (60) amefariki kutokana na Kubakwa na mtu zaidi
ya mmoja ambapo mpaka wanafanya uchunguzi wamekuta sehemu za siri za marehemu
zikitoka damu.
|
Mwanamke mmoja mkaziwa kitongoji cha Mukididili katika Mamlaka ya mji mdogo wa Ngara mkoani Kagera amekutwa amefariki dunia baada ya kufanyiwa tendo la ubakaji na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia May 19,2014.
Kamanda wa
jeshi la Polisi mkoani Kagera George Mayunga
amemtaja mwanamke huyo kuwa ni Jenni
Furuguti (60) ambaye alikutwa
jana(May 19,2014) jirani na eneo la
uwanja wa tenki la maji katika kitongoji hicho majira ya saa saba usiku.
Kamanda Mayunga
amesema mwanamke huyo kabla ya kupatwa
na mauti alikuwa katika starehe za kawaida kwa kupata kinywaji (pombe) na
wakati anarejea nyumbani ndipo alikutana na watu hao na kumfanyia unyama huo.
Ameongeza
kuwa ,kutokana na tukio hilo tayari mwanamke mmoja ambaye amekutwa na simu ya
marehemu anashikiliwa na jeshi la Polisi wilayani Ngara kwa mahojiano zaidi
kufuatia kifo hicho na uchunguzi unaendelea ili kubaini wahusika wengine.
Kamanda
Mayunga amesema katika eneo la tukio kunaonyesha kuwa kulikuwa na purukushani zilitokea na kwamba
haikuwa rahisi kwa mwanamke huyo kujinasua na hivyo kubakwa ingawa katika
sehemu ya mwili wake hapakuonesha michubuko ama majeraha.
Aidha
Taarifa za Daktari aliyeufanyia Uchunguzi mwili wa Marehemu,Dr.Daniel Dankani
amesema kuwa ,Marehemu Jenni Furuguti (60)amefariki kutokana na Kubakwa na mtu zaidi
ya mmoja ambapo mpaka wanafanya uchunguzi wamekuta sehemu za siri za marehemu
zikitoka damu.
Wakati huo
huo msichana mmoja Furaha Denis (16)aliyekuwa akifanya kazi za
ndani eneo la Ngara mjini mkoani Kagera amejinyonga hadi kufa
kwa kutumia kipande cha kanga nyumbani kwa mwajiri wake.
Kaimu Mwenyekiti
wa kitongoji cha Ngara mjini Thomas Milenzo amesema msichana huyo ni mzaliwa wa kijiji
cha Mabawe wilayani Ngara na kwamba
tukio hilo limetokea May 17,2014, majira ya saa 1 usiku nyumbani mwajiri wake
ambaye ni Baruani Mbwana.
Jeshi la
polisi Mkoani Kagera limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hilo ni
tukio la nne kwa wilaya hiyo ndani ya mwezi huu wa tano la watu kujinyonga na matukio mengine yanahusishwa na Imani za Ushirikina.
No comments:
Post a Comment