Tazama Taswira ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Dr. Martin Luther King Jr. jijini Washington. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, August 29, 2013

Tazama Taswira ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Dr. Martin Luther King Jr. jijini Washington.

Rais Barack Obama wa Marekani akitoa hotuba wakati wa kuadhimisha miaka 50 ya maandamano ya kutetea haki za kiraia na hotuba ya kihistoria ya  Martin Luther King Jr. "I have a dream" kwenye makumbusho ya  Lincoln jijini Washington, Aug. 28, 2013.

Kuanzia kushoto, Rais wa zamani Jimmy Carter, rais wa zamani Bill Clinton, balozi wa zamani kwenye Umoja wa Mataifa  Andrew Young, mke wa rais Michelle Obama, na Rais Barack Obama wakisimama wakati wa wimbo wa taifa kuadhimisha miaka 50 ya Mandamano kuelekea Washington,  Aug. 28,2013.

Wanawake watatu waliohudhuria maandamano yaliyopita, kutoka kushoto  Armanda Hawkins wa Memphis, Vera Moore wa Washington, na Betty Waller Gray wa Richmond, Va., (anaebeba bango ) linawasikiliza wageni waheshima wakitoa hotuba wakati wa mandamano ya Washington, Aug. 28, 2013, kwenye makumbusho ya  Lincoln Memorial.

The group Junkaroo performs at the Let Freedom Ring ceremony at the Lincoln Memorial in Washington, Aug. 28, 2013, to commemorate the 50th anniversary of the 1963 March on Washington for Jobs and Freedom.

Crowds gather on the National Mall to commemorate the 50th Anniversary of the March on Washington, August 28, 2013.

Martin Luther King III speaks during a ceremony marking the 50th anniversary of his father Martin Luther King, Jr.'s "I Have a Dream" speech on the steps of the Lincoln Memorial in Washington, August 28, 2013. 

President Barack Obama, first lady Michelle Obama, former president Bill Clinton and former president Jimmy Carter arrive at the Let Freedom Ring ceremony at the Lincoln Memorial, Aug. 28, 2013, to commemorate the 50th anniversary of the 1963 March on Washington.

Former presidents Jimmy Carter and Bill Clinton arrive at the Let Freedom Ring ceremony at the Lincoln Memorial in Washington, Aug. 28, 2013.

Actor Jamie Foxx speaks during a ceremony marking the 50th anniversary of Martin Luther King, Jr.'s "I Have a Dream" speech on the steps of the Lincoln Memorial in Washington, August 28, 2013. 

A woman stands in the crowd taking part in the anniversary of the March on Washington, August 28, 2013. (R. Green/VOA)


Miaka  hamsini iliyopita Mchungaji Martin Luther King Junior aliongoza maandamano yaliyobadilisha maisha ya wamarekani wote. Mnamo Agosti 28 mwaka wa 1963, King alitoa hotuba yake maarufu ‘ I Have a Dream” kwa umati  mkubwa  wa zaidi ya watu laki mbili na nusu hapa Washington. Tukio hilo lilibadilika kuwa la kihistoria nchini Marekani.

Watu robo milioni waliandamana kutetea haki sawa na ajira. Maandamano hayo yalifanyika wakati wa ghasia kubwa za ubaguzi wa rangi huku Marekani ikitafuta ufumbuzi wa sheria zake zilizobagua  wamarekani weusi wenye asili ya Kiafrika.

Mchungaji Jesse Jackson anasema Martin Luther King alikuwa na maono sahihi juu ya  maandamano hayo ya kihistoria.

Waliohudhuria mkusanyiko huo wanasema ulikuwa  wa kisherehe. Wasomi wengi wa historia wanakubaliana kuwa maandamano hayo yalitoa ujumbe mzito kwamba  sharti ubaguzi wa rangi ufike kikomo.

Mchungaji Willie Blue anasema hakutegemea tukio hilo lingekuwa la uzito ule.

Dr. Martin Luther King Jr.
akitoa hotuba Aug 28,1963
Dr. King alitumia mkusanyiko huo mkubwa wa watu kutoa hotuba yake maarufu, I have a  dream akieleza kuwa ana ndoto, kwamba watu wote duniani waliumbwa sawa.

Aliashiria shida za Wamarekani weusi wakijaribu kupigana dhidi ya ubaguzi wa rangi. Lakini  kilele cha hotuba ya Dr. King  kilikuwa pale alipoelezea kuhusu maazimio binafsi ya taifa la Marekani.

 Nina ndoto kuwa wanangu wanne  siku moja wataishi katika taifa ambalo maamuzi juu yao hayatafanywa kwa misingi ya rangi yao, lakini kwa matendo ya tabia zao. Nina ndoto leo

Mbunge wa Marekani John Lewis ambaye alizungumza wakati wa maandamano hayo, anasema matamshi ya Dr. King yanasisimua. Alisema “Alibadili ngazi zinazoelekea kwenye mnara wa kumbukumbu wa Lincoln kuwa kama  eneo la mchungaji anapohubiri na namkumbuka akisema  nitaota leo, ndoto inayokita mizizi yake kwenye ndoto za Marekani.”

Naye Dick Miles alikuwa miongoni mwa wazungu wengi walioshiriki maandamano hayo.alisema hakudhani kuna mmoja wao aliyetegemea hotuba ya kusisimua kama waliyoisikia. ‘Iligusa kila mmoja moyoni.”

Maandamno ya Washington yalimalizika  Dr. King akiwaomba wamarekani wote wakubali uhuru utawale.

Mbunge John Lewis anakumbuka kuwa watu walipoanza kurejea makwao, viongozi wa haki za kiraia walikutana White House na rais John Kennedy ambaye aliwaalika White House. 

Lewis alimwelezea rais Kennedy  kama baba aliyefurahia vitendo vya wanawe; ‘alitwambia kila mmoja, ‘mmefanya kazi nzuri, na alipomfikia Dr. King, akasema ‘na wewe ulikuwa na ndoto.”

King alisema maandamano hayo yatakuwa mojawapo ya maandamano makubwa katika historia  ya kutetea uhuru na hadhi ya binadamu kuwahi kufanyika Marekani.

Wasomi wa historia wanasema maandamano hayo ya Washington yalikuwa ya amani na bila shaka yoyote yalibadilisha taifa la Marekani.



Rais Barack Obama.

Akizungumza na maelfu ya watu waliohudhuria maadhimisho ya miaka 50 tangu maandamano ya kutetea haki za kiraia kufanyika jijini Washington, rais Barack Obama jana(Agosti 28,2013) Jumatano alisema ‘kazi haijamalizika’ ya kutetea haki na usawa kwa wamarekani wote.

Miaka 50 baada ya  Mchungaji Martin Luther king Jr. kutoa hotuba ya kihistoria na ya kusisimua akisema; “I have a dream” wakati wa ubaguzi mkubwa wa rangi Marekani, rais wa kwanza mweusi Marekani alisimama katika ngazi zile, zile alizosimama kwenye mnara wa kumbukumbuku wa  Lincoln Memorial.

Bw. Obama alielezea wasifu wa Dr.King pamoja na kujitolea kafara kwa walioshiriki maandamano makubwa ya Washington miaka 50 iliyopita. 

Alisema kutokana na maandamano yao, sheria ya haki za kiraia ilipita. Na kwa sababu waliandamana  sheria  ya haki za kupiga kura ilitiwa saini na kwa sababu hiyo hiyo wasichana na wavulana weusi wanaweza  kuishi maisha yao kikamilifu bila kuwa watumwa wa mtu mwingine.

Rais Obama aliendelea kusema na kwa sababu waliandamana, hata White House imebadilika huku maelfu ya watu wakimshangilia. Bw. Obama alisema maandamano hayo yalileta haki sio tu kwa wamarekani weusi lakini kwa watu wa rangi nyingine Marekani na duniani waliokuwa na kiu cha kuwa huru.

Alisema mengi yamebadilika tangu maandamano hayo ya mwaka wa 1963 lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanywa. Alisema kuna mwanya mkubwa kati ya matajiri na maskini miongoni mwa watu wa rangi mbalimbali Marekani na migawanyiko mikubwa ya kisiasa hapa Washington inayofanya ndoto ya Martin Luther King Jr. kuonekana kuwa mbali sana kutimia.

Rais Obama alisema Marekani ina chaguo, ama kuendelea na msukumo huu mkubwa wa kidemokrasia, au kuzembea na kukifanya kizazi kijacho kuishi bila matumaini au kujikakamua na kufanya mabadiliko ya kuleta usawa na haki kwa wote.

Orodha ya waliotoa hotuba katika maadhimisho hayo ilikuwa ndefu, na ilijumwisha mwana wa kike wa  Dr. King, mchungaji Bernice King, marais wa zamani Bill Clinton, Jimmy Carter, wacheza sinema maarufu na hata watangazaji mashuhuri wa televisheni. Mbunge John Lewis mmoja wa viongozi wa maandamano ya kutetea haki za kiraia mwaka wa 1963 alisema  ingawa  kuna maendeleo, ubaguzi wa rangi ungali umejikita katika jamii ya wamarekani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad