Mnamo tarehe
20/08/2013 majira ya 08.45 hrs. huko katika kijiji cha Fufu, Kata ya Fufu,
Wilaya ya Chamwino, takribani magari matano (5) yaliyokuwa kwenye msafara wa
Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea kwenye makabidhiano Wilaya
ya Mpwapwa, moja ya magari yaliyokua kwenye msafara huo lilikutana na tuta huku
dereva wake akishika ‘brake’ ghafla na kusababisha magari yaliyokuwa nyuma yake
kugonga gari la mbele kwa kila moja lililokuwa likitimka kutokana na vumbi
kubwa lililokuwa likifuka wakati wa msafara huo kufuatia matengenezo ya
barabara Dodoma – Iringa yanayoendelea.
Katika ajali
hiyo magari yaliyoathirika ni kama ifatavyo:-
1. STK 3007
TOYOTA LAND CRUISER
2. STK 3357
TOYOTA LAND CURISER yote ni mali ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa Katibu Tawala [M]
Dodoma.
3. SM 5835
TOYOTA LAND CRUISER mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.
4. DFP.7178
TOYOTA LAND CRUISER (AMBULANCE) nayo ikiwa ni mali ya Halmashauri ya Manispaa
ya Dodoma.
5. T.627 BFJ
TOYOTA LAND CRUISER mali ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma.
6. STK 4983
TOYOTA LAND CRUISER HARD TOP Mali ya Wizara ya Kilimo.
Watu wapatao tisa (9)
walijeruhiwa katika ajali hiyo, kati yao wanne (4) wamelazwa katika Hospitali
ya Rufaa Dodoma na watano (5) walipatiwa matibabu na kuruhusuiwa kurudi
nyumbani.
Majeruhi
waliolazwa ni kama ifuatavyo:-
Majeruhi. |
1. JUMA S/O
ALLY @ SIMAI, Miaka 32, Mpemba, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Mkazi wa
Kusini Unguja.
2. CHARLES
S/O MAMBA, Mgogo, Miaka 50, Mkazi wa Ipagala, Diwani wa Kata ya Ipagala.
3. DATIVA
D/O KIMOLO, Miaka 46, Mrangi, Afisa Mifugo, Manispaa ya Dodoma, Mkazi wa
Mailimbili.
4. AMINA D/O
MGENI, Miaka 36, Muuguzi Kituo cha Afya Makole, Mkazi wa Area ‘C’ Manispaa ya
Dodoma.
Majeruhi
waliotibiwa na kuruhusiwa kurudi makwao ni kama ifuatavyo:-
1. JACKLINE
D/O MAGOTI, Miaka 39, Mjita, Muuguzi Kituo cha Afya Makole, Mkazi wa Area C
Manispaa ya Dodoma.
2. RICHARD
S/O MAHELELA, Miaka 51, Mgogo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Ipagala, Mkazi wa Ipagala
Manispaa ya Dodoma.
3. JUMANNE
S/O NGEDE, Miaka 58, Mrangi, Diwani Kata ya Chamwino/ Naibu Meya wa Manispaa ya
Dodoma, Mkazi wa Chamwino Manispaa ya Dodoma.
4. ZAITUNI
D/O VARINOI, Miaka 43, Mkazi wa Mbwanga, Manispaa ya Dodoma.
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Dodoma linatoa wito kwa madereva na watumiaji wa barabara
hususani zilizopo kwenye matengenezo wanapokuwa katika misafara, wanapaswa kuwa
makini na wapeane nafasi kati ya gari moja hadi jingine ili kuepusha madhara
yanayoweza kuepukika.
No comments:
Post a Comment