Kampuni ya Vodacom yakabidhi vifaa kwa timu 14 shiriki za ligi kuu Tanzania bara 2013/2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, August 21, 2013

Kampuni ya Vodacom yakabidhi vifaa kwa timu 14 shiriki za ligi kuu Tanzania bara 2013/2014.

Wawakilishi wa timu mbalimbali zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya michezo na mdhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom tayari kwa ajili ya kuanza kwa msimu wa ligi kuu 2013/2014. Pamoja nao katika picha ni Mkuu  wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa kampuni  hiyo Kelvin Twisa,(Aliyeshikilia mpira) na Mkurugenzi  wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba.
Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Tanzania Bara Kampuni ya Vodacom leo imekabidhi vifaa kwa timu 14 shiriki za ligi hiyo vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh 400 Milioni.

Akizungumza kabla ya zoezi la kukabidhi vifaa hivyo kuanza, Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba pamoja na kuishukuru Vodacom kwa kutekeleza majukumu yake ya kimkataba amevitaka vilabu vya ligi kuu kuu ya Vodacom kuheshimu chapa ya mdhamini wakati wote wa mechu za ligi.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa alisema kuwa vifaa hivyo viko tayari na anaamini timu zote zimejiandaa vya kutosha na tayari kuingia katika mtanange wa ligi.

“Tunajisikia furaha sana kufikia hapa leo na kukabidhi vifaa hivi tukitekeleza matakwa ya mkataba wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu zineshajiandaa vizuri na sasa tupo tayari kuanza msimu mpya wa 2013/2014.’Alisema Twissa.


Twissa aliongeza kuwa vifaa vipya vilivyo kabidhiwa ni pamoja na seti za jezi mbalimbali, viatu vya mazoezi na mechi, soksi, vilinda ugoko (shin guards), nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves na vifaa vingine. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad