Shekh
Ponda akisisistiza jambo mbele ya waumini wa Dini ya Kiislamu kwenye Kongamano
, Augosti 10, mwaka huu mjini Morogoro.
|
Hapa ni Kutambulishwa
jukwaani Shekh Ponda.
|
Askari wa FFU wakijisongeza kati kati ya uwanja mara baada ya
muda wa kongamano kumalizika na huu ndio mwanzo wa patashika lililompata Sheikh
Ponda.
|
Shekh Ponda akikaribishwa kwenye jukwaa kuu baada ya kuwasili kwenye viwanja vya shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege , mjini Morogoro hapo jana Agosti 10,2013. |
Shekh Ponda akisalimiana na Mhadhiri wa Mihadhara
nchini, Ustaadhi Abubakari.
|
Hali ya
wasiwasi imetanda mjini Morogoro baada ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, kudaiwa kupigwa risasi begani wakati
polisi wakiwa katika harakati ya kumkamata.
Habari
kutoka katika eneo hilo zinadai kuwa Ponda alipigwa risasi saa 12:25 jioni,
wakati akisindikizwa na wafuasi wake kuelekea katika Msikiti wa Mungu Mmoja
Dini Moja, baada ya kumaliza kutoa mhadhara katika kongamano lilifanyika mjini
Morogoro jana(Agosti 10,2013.
Tukio hilo
lilitokea katika Barabara ya Tumbaku, baada ya kumalizika kwa mkutano wa
kongamano lililoandaliwa na Jumuiya ya Wahadhiri wa Kiislamu Mkoa wa Morogoro.
Mwenyekiti
wa Kongamano hilo, Sheikh Idd Mussa Msema aliliambia Mwananchi Jumapili jana
kuwa Ponda alipigwa risasi sehemu ya bega, na askari polisi na kwamba
aliwahishwa kutibiwa katika Hospitali ya Kiislamu iliyopo eneo Msamvu mjini
Morogoro.
Hata hivyo,
wakati Sheikh huyo akisema hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine
Shilogile alikanusha madai ya kuwa polisi wamempiga risasi.
Alisema
polisi walifika katika eneo hilo kwa ajili ya kumkamata Ponda, baada ya
kumaliza mhadhara wake na kwamba wakati wakitaka kumkamata ndipo wafuasi wake
wakawazuia polisi na kulazimika kupiga mabomu ya machozi na risasi hewani
kuwatawanya.
Katika tukio
hilo inadaiwa kuwa Sheikh Ponda aliyekuwa katika gari ndogo huku wafuasi wake
wakimsindikiza kwa miguu, walipofika eneo la gereji mabomu ya machozi yalipigwa
na polisi waliokuwa katika magari aina ya defender wakati wakijaribu
kuwatawanya wafuasi hao.
Baada ya
tukio hilo baadhi ya wafuasi wake walimchukua Sheikh Ponda kutoka katika gari
lake na kumkimbizia katika gereji moja, kisha wakatoka wakiwa wamempakia katika
pikipiki na kumpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro.
Mlinzi mmoja
wa lango namba moja alisema kuwa ulifika msululu wa pikipiki zaidi ya 50,
lakini pikipiki zote zilizuiliwa isipokuwa iliyokuwa imembeba Sheikh Ponda na
kwenda naye mpaka mapokezi.
Aidha,
alisema wakiwa katika eneo hilo magari kadhaa ya polisi yaliingia katika lango
la hospitali hiyo. Hivyo wafuasi wa Sheikh Ponda wakalazimika kumbeba begani na
kutoroka naye kupitia lango namba mbili.
Taarifa
zilizopatikana baadaye zinadaiwa kuwa Sheikh Ponda alikimbizwa katika Hospitali
ya Kiislamu ya Msamvu.
Baadhi ya
watu walidai kumwona Sheikh Ponda akiingizwa katika Hospitali ya Rufaa
Morogoro, lakini walishangaa alivyotoweka.
Habari Na:Mwananchi.
Umati wa waumini wa
Kiislamu wakimsikiliza Shekh Ponda.
|
Waumini wa Dini ya Kiislamu wa mjini Morogoro wakimsikiliza Shekh Ponda. |
Waumini wa Kiislamu wakitawanyika uwanjani baada ya
muda wa kongamano kufikia tamati.
|
HAPA CHINI
KUNA USHUHUDA WA MDAU ALIYEKUWA ENEO LA TUKIO KAMA ALIVYOUANDIKA KATIKA MTANDAO
WA JAMII FORUM:
Kweli
nimeshindwa kuamini kilichotokea, Sheikh Ponda kupigwa risasi. Nilikuwepo pale
uwanjani tena nilikuja mapema kabisa na hivyo kushuhudia kila kitu
kilichotokea.
Kimsingi
sikuona sababu ya Sheikh Ponda kutokewa na tukio baya kiasi kile ambacho
hakionyeshi ubinaadamu kabisa, utu wetu, uhuru wetu na hata heshima tuliyonayo
Watanzania kwenye jumuiya za kimataifa. Mpaka sasa haieleweki ni nani hasa
kampiga risasi Sheikh Ponda, lakini minong'ono ya watu wanasema ni polisi
wamehusika.
Binafsi
pamoja na kufuatilia kwa ukaribu sikuona ilikotokea risasi hata aliyepiga na
nilikuwa mbali kidogo na tukio. Ila nilimwona wakati anapandishwa kwenye
pikipiki akiwa tayari amekwisha kupigwa risasi. Imewahuzunisha wengi!
Jamaa
ameongea kwa muda mfupi sana ni takribani dakika 18, kwani alianza kuongea saa
11:54 na alimaliza kuongea saa 12:12 jioni.
Hali ya
uwanjani kwa kweli ilikuwa shwari sana, hata polisi hawakuonekana jirani
walikuwa kwa nyuma kabisa huku wakiwa wamejisheheni kwa zana zote za kazi.
Mara baada
ya Ponda kukaribia kumaliza kuongea alisema kuwa muda hautoshi isipokuwa
alitangaza kuwa kesho baada ya swala ya adhuhuri atakuwa kwenye msikiti wa mkoa
wa Morogoro wa Boma Road ambapo ataongea kwa kirefu hivyo kuwataka Waislamu
kesho kuhudhuria eneo hilo.
Inavyooneka
polisi walipanga wamkamate hata kabla ya kuongea katika ule mkutano na ndiyo
maana walitega sehemu kana kwamba walikuwa wakimsubiri aingie wamkate.
Lakini
katika hali isiyotarajiwa na wengi, Sheikh Ponda iliingia uwanjani kupitia
upande wa pili ambapo msafara wake ulikuwa na gari moja tu na taksi mbayambaya
kiasi kwamba wala huwezi kudhania.
Mara tunashangaa gari imesimaa na Sheikh Ponda
na Amiri wa Wahadhiri Tanzania Sheikh Kondo Bungo wakashuka, wakapita kwenye
kundi la Waislam kwa nyuma ghafla kivumo cha shangwe na Takbir kikavuma huku
umati wa Waislam waliohudhuria hapo ukiitia Allah Akbar, Allah Akbar n.k.
Wakati huo
jukwaani alikuwa akiongea Sheikh Said Riko na ndiyo aliyewapokea kwa kuanzisha
Takbir ambayo iliitikiwa na Waislam Allahu Akbar, Allah Akbar. Kwa sababu
waliingia kwa kuchelewa ilibidi mara moja Sheikh Said Rico ampishe Sheikh Kondo
Bungo, Amiri wa wahadhiri Tanzania aongee.
Wakati
anaendelea kuongea kabla hata hajamaliza umeme ukakatika, likachukuliwa
jenereta ambalo lilikuwa jirani likawashwa, na mhadhara ukaendelea kama
kawaida.
Sheikh Kondo
Bungo akamaliza mada yake, akarudi Sheikh Said Riko, akaongea na kuchangisha
michango kwa ajili ya kuendeleza harakati kwa muda wa kama dakika tano hivi
ndipo akaruhusiwa Sheikh Ponda kupanda jukwaani.
Sheikh Ponda
mara baada ya kumaliza kuongea, watu wakaanza kutawanyika, lkn ghafla mwendesha
shughuli akatangaza waislam wasitawanyike kwanza kwa kuwa kulikuwa na
matangazo.
Wakati
matangazo yanendelea ambayo sikuweza kuyasikia , ghafla tukaona defenda moja ya
polisi inaingia ambayo ilikuwa imejaza polisi walio tayari kwa mapambano.
Waislam wakawa wanawashanga kulikoni tena ilhali mkutano ulifanyika na kuisha
kwa amani kabisa.
Basi Sheikh
Ponda akaingizwa kwenye taxi iliyokuja kumfuata akiambatana na Sheikh Kondo
Bonge.
Polisi
walitaka kumkamata Sheikh Ponda lakini waumini wakamkinga kwa kulizingira gari
alilopanda huku likiondoka taratibu. Huku nyuma gari la polisi likawa linafuata
taratibu bila kupiga risasi hewani wala kupiga mabomu ya machozi.
Gari ya
polisi ilipofika barabara ya lami maeneo ya karibu na jengo la Fire ilionekana
kusimama kwa muda huko gari iliyombeba Sheikh Ponda kukunja kushoto kuelekes
kwenye msikiti wa Mungu mmoja dini moja.
Kabla
msafara wa Ponda haujafika kokote gari nne za polisi zilikuja kwa kasi sana na
kuanza kupiga mabomu ya machozi kuwatawanya waumini, watu walitawanyika na
Sheikh Ponda akashuka na kuelekea kwenye gereji moja hivi kabla ya kufika idara
ya maji ambako ndiko alikopigwa risasi.
Kwa kweli
sijui ilikotokea risasi iliyompiga Ponda, nadhani kamanda wa polisi atalitolea
ufafanuzi zaidi. Mimi nimeandika kile nilichoona kwa macho yangu!
Mi nilidhani
ingekuwa busara kwa jeshi la polisi kama walimuhitaji Sheikh Ponda wangemwambia
anahitajika polisi na hivyo ajisalimishe.
Na Mdau
No comments:
Post a Comment