Mtu mmoja amefariki na wengine 15 kujeruhiwa baada ya basi la Hood kumgonga mtembea kwa miguu na kisha kupinduka. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, August 28, 2013

Mtu mmoja amefariki na wengine 15 kujeruhiwa baada ya basi la Hood kumgonga mtembea kwa miguu na kisha kupinduka.



Mtu mmoja amefariki Dunia na wengine 15  wamejeruhiwa baada ya basi  la Kampuni ya Hood  lililokuwa likitokea  wilayani Kilombero kwenda jijini  Dar es salaam kumgonga  mtembea kwa miguu na kisha kuacha njia na kupinduka katika eneo la Kiembeni  Mikese Mkoani  Morogoro.


Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro Bw. Bonifasi Mbao  akizungumza kwenye  eneo la tukio leo(Agosti 28,2013) amesema chanzo cha ajali  hiyo ni mwendo kasi ambapo dereva wa basi  gari  ilimshinda na kugonga mtembea kwa miguu na kisha kupinduka ambapo  dereva wa basi amekimbia mara baada ya tukio la ajali.

Basi  la Kampuni ya Hood likiwa limeacha  njia na kupinduka katika eneo la Kiembeni  Mikese Mkoani  Morogoro  baada ya kumgonga  mtembea kwa miguu leo (Agosti 28,2013)

Taarifa za  madaktari  katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro  zimeeleza  majeruhi wanaendelea na matibabu na mwili wa marehemu umehifahiwa katika chumba cha maiti hospitali ya mkoa wa Morogoro .

Chanzo  Na: ITV

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad