Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Tanzania
Bara Kampuni ya Vodacom leo imekabidhi vifaa kwa timu 14 shiriki za ligi hiyo
vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh 400 Milioni.
Akizungumza kabla ya zoezi la
kukabidhi vifaa hivyo kuanza, Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba
pamoja na kuishukuru Vodacom kwa kutekeleza majukumu yake ya kimkataba
amevitaka vilabu vya ligi kuu kuu ya Vodacom kuheshimu chapa ya mdhamini wakati
wote wa mechu za ligi.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha
Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa alisema kuwa vifaa hivyo viko
tayari na anaamini timu zote zimejiandaa vya kutosha na tayari kuingia katika
mtanange wa ligi.
“Tunajisikia furaha sana kufikia
hapa leo na kukabidhi vifaa hivi tukitekeleza matakwa ya mkataba wa udhamini,
ni imani yetu kwamba timu zineshajiandaa vizuri na sasa tupo tayari kuanza
msimu mpya wa 2013/2014.’Alisema Twissa.
Twissa aliongeza kuwa vifaa vipya
vilivyo kabidhiwa ni pamoja na seti za jezi mbalimbali, viatu vya mazoezi na
mechi, soksi, vilinda ugoko (shin guards), nguo za mazoezi, nguo za kawaida,
gloves na vifaa vingine.
No comments:
Post a Comment