Arsenal imefuzu kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kiulaini ikiitoa Fenerbahce. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, August 28, 2013

Arsenal imefuzu kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kiulaini ikiitoa Fenerbahce.

Arsenal imefuzu kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa usiku huu, kiulaini ikiitoa Fenerbahce.

Arsene Wenger sasa anatakiwa hadi usiku wa Jumatatu kumaliza tatizo lake sokoni kwa kununua wachezaji.

Mabao mawili ya Aaron Ramsey Uwanja wa Emirates katika dakika za 24 na 72 usiku huu yameifanya Arsenal iwatoe Waturuki kwa jumla ya 5-0 baada ya awali kushinda 3-0 ugenini. 

Sasa Arseenal wanaungana na Mabingwa wa England, Manchester United, Manchester City na Chelsea, kwenye Droo ya kupanga Makundi ya UEFA Champions League itakayofanyika Agosti 29 huko Monaco.

Pamoja na Arsenal, Timu nyingine zilizofuzu kuingia hatua ya Makundi hiyo Jana ni Schalke, walioifunga PAOK ya Ugiriki Bao 3-2, Steau Bucharest, ilitoyoka Sare Mechi zote mbili na Legia Warsaw na wao kusonga kwa Goli za Ugenini, Basel na FK Austria Wien.

UEFA Champions League. 

RAUNDI YA MCHUJO-Mechi za Marudiano 
Jumanne Agosti 27,2013.

[Kwenye Mabano Jumla ya Magoli Mechi mbili]

PAOK FC - Greece 2 Schalke 04 – Germany 3 [3-4]

Legia Warsaw - Poland 2 FC Steaua Bucuresti – Romania 2 [3-3, Steau wasonga Gola za Ugenini]

FC Basel 1893 - Switzerland 2 Ludogorets Razgrad – Bulgaria 0 [6-2]

FK Austria Wien - Austria 2 NK Dinamo Zagreb – Croatia 3 [4-3]

Arsenal FC - England 2 Fenerbahçe – Turkey 0 [5-0]

Leo zipo Mechi nyingine 5 za Raundi ya Mchujo ambazo Washindi wake watano wataungana na Washindi watano wa Jana na Timu 22 zilizopitishwa moja kwa moja kwenye Droo ya kupanga Makundi ya UEFA Champions League.

UEFA Champions League
RAUNDI YA MCHUJO-Mechi za Marudiano

[Saa za Bongo] 
Jumatano Agosti 28,2013.

[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya kwanza]

19:00 Zenit St. Petersburg - Russia v Pacos Ferreira – Portugal [4-1]

21:45 Celtic – Scotland v Shakhter Karagandy - Kazakstan [0-2]

21:45 AC Milan – Italy v PSV Eindhoven - Netherlands         [1-1]

21:45 Real Sociedad - Spain v Olympique Lyonnais - France [2-0]

21:45 NK Maribor - Slovenia v FC Viktoria Plzen - Czech Republic [1-3]


KLABU 22 ZINAZOANZA MOJA KWA MOJA HATUA YA MAKUNDI.

-Bayern Munich

-Atlético Madrid

-Benfica

-Shakhtar Donetsk

-Manchester United

-Borussia Dortmund

-Paris Saint-Germain

-Olympiacos

-Manchester City

-Bayer Leverkusen

-Marseille

-Galatasaray

-Chelsea

-Juventus

-CSKA Moscow

-Anderlecht

-Barcelona

-Napoli

-Ajax

-FC Copenhagen

-Real Madrid

-Porto

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad