![]() |
| Yanga SC |
Kwa Matokeo
hayo yanaifanya Yanga SC itimize pointi 36 baada ya kucheza mechi 16, ikiwazidi Azam FC pointi 33 katika nafasi ya pili na mabingwa watetezi,
Simba SC wanashika nafasi ya tatu kwa pointi zao 28.
Hadi
mapumziko, Yanga SC walikuwa tayari wanaongoza
kwa mabao 2-0 ambayo yote yalitiwa
kimiani na Jerry Tegete.
Hamisi Kiiza
alikosa penalti dakika ya 47 baada ya
kipa Abdul Seif kudaka, kufuatia beki Ibrahim Job kumchezea rafu Haruna
Niyonzima kwenye eneo la hatari.
Didier
Kavumbangu aliyeingia kuchukua nafasi ya Jery Tegete aliifungia Yanga bao la
tatu kwa penalti dakika ya 69, baada ya beki Sunday Bakari kuunawa mpira kwenye
mpira eneo la hatari.
Yanga
ilihitimisha karamu yake mabao kupitia
kwa kiungo Nizar Khalfan aliyeingia kipindi cha pili pia kuchukua nafasi ya
Simon Msuva, aliyefunga bao la nne dakika ya 80 kwa shuti akiunganisha krosi ya
Saidi Bahanuzi, aliyetokea benchi pia kumpokea Kiiza.
Yussuf
Mlipli alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 90, baada ya kumchezea rafu David
Luhende.
Katika mechi
nyingine za Ligi kuu soka Tanzania bara, Toto African ilitoka 2-2 na Polisi
Moro kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wakati Mtibwa Sugar nayo
imelazimishwa sare 0 – 0 na Ruvu
Shooting kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.






No comments:
Post a Comment