Sigara. |
Wanaelezea
kuwa saratani ya mapafu ndio imekuwa sasa saratani nambari moja ambayo inasababisha
vifo miongoni mwa wanawake ambapo Hali hiyo tayari inashuhidiwa nchini Uingereza na
Poland.
Kulingana
na watafiti, hii ni ishara ya idadi kubwa ya wanawake wanaovuta sigara hali
iliyoanza kujitokeza kuanzia mapema miaka ya tisini na sabaini.
Idadi
ya vifo vinavyotokana na saratani ya mapafu, vitaendelea kuongezeka katika
miaka ijayo, lakini sasa kwa sababu ya vijana wa kike wasiovutiwa na kuvuta
sigara na ambao idadi yao sio kubwa sana , huenda vifo hivyo vikapungua.
Mwaka
2013, takriban wanawake 82,640 barani Ulaya watafariki kutokana na saratani ya
mapafu ikilinganishwa na wanawake 88,886 watakaofariki kutokana na saratani ya
matiti.
Sigara. |
Wanatarajiwa
kuwa vifo vinvyotokana na saratani ya mapafu kupungua mwaka 2020 au 2025 kwa
sababu angalu vijana wa kiike hawavuti sana sigara.
Lakini
ifikapo mwaka 2015, wanawake wengi watafariki kutokana na saratani ya mapafu
kuliko saratani ya matiti, kulingana na mtaalamu wa afya ya wanawake, Profesa
Carlo La Vecchia .
Takwimu
zinaonyesha kuwa ingawa watu wengi zaidi wanaugua saratani, kwa sababu wanaishi
muda mrefu zaidi,ni watu wachache sana wanafariki kutokana na saratani.
Licha
ya kupungua kwa idadi ya watu wanaofariki kutokana na saratani barani humo,
idadi ya wanawakewanaofariki kutokana na saratani ya mapafu inaongezeka katika
nchi zote za Ulaya.
Profesa
La Vecchia,wa chuo kikuu cha Milan, Italy, anasema kuwa hali hii inaleta
wasiwasi kwa sababu hakuna dalili kuwa ugonjwa huo unapungua.
Uvutaji
sigara pamoja na ugonjwa wa sukari ndio vinachangia kuongezeka kwa ugonjwa huu.
Lakini wataalamu wanasema bado hawajui nini kinasababisha sehemu kubwa ya
saratani hiyo.
Wataalamu
wanasema kuna umuhimu wa wanawake kuwacha kuvuta sigara.
Stori Na:BBC.
No comments:
Post a Comment