Baadhi ya
wazazi wamesema kuwa wamepokea taarifa za radi hiyo kwa mstuko mkubwa,
kwasababu idadi ya watoto hao zaidi ya 60 waliojeruhiwa sambamba na walimu wao
wawili wa kike siyo la kawaida, na kwamba baadhi ya watoto walioruhusiwa kurudi
nyumbani hawako kwenye hali ya kawaida, wengine wakitembea kwa kuchechemea
ilhali wengine wakiwa na hofu ya kutokea tena tukio kama hilo.
![]() |
|
Katibu wa
hospitali ya mkoa wa Kagera Kilwanila
Kiiza, amethibitisha kuwapokea
majeruhi kadhaa saa tatu asubuhi, ambapo kati ya hao wawili walikuwa
wamepoteza fahamu, na kati ya 7 waliolazwa wawili ni wawilimu na watoto watano.
Amesema kuwa
wamejitahidi kuwapa huduma ya mazoezi ya kupunguza mionzi miilini, na
wataendelea na uangalizi wa karibu kwa saa 24, akiwataja walimu kuwa ni
Mwl.Witnes Kabyemela na mwl.Theodata Prosper, na kwamba wanafunzi waliolazwa ni
wa darasa la pili hadi la saba.
|








No comments:
Post a Comment