Taswira ya Kili Music Tour 2013 na kupata shangwe kubwa toka kwa mashabiki wa mkoa Kigoma. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, September 02, 2013

Taswira ya Kili Music Tour 2013 na kupata shangwe kubwa toka kwa mashabiki wa mkoa Kigoma.

Ziara ya wanamuziki waliofanya vizuri mwaka 2012 maarufu kama Kilimanjaro Music Tour 2013 iliyopewa kaulimbiu ya Kikwetu kwetu imefanyika mkoani Kigoma Jumamosi(Agost 31,2013) na kuvunja rekodi ya mahudhurio katika uwanja wa Lake Tanganyika baada ya maelfu ya wakazi wa mji wa Kigoma na maeneo ya jirani kufurika kwa wingi kuwashuhudia wasanii wakali 12 waliopanda jukwaani. 
Kivutio kikubwa katika tamasha hilo ilikuwa ni wanamuziki wanne wanaounda kundi la Kigoma All Stars, Diamond, Mwasiti, Linex na Recho kupanda mwishoni na kuimba wimbo wao maarufu wa Leka Dutigite na kupata shangwe kubwa toka kwa mashabiki. 
Hizi ni baadhi ya picha za matukio yaliyotokea.














Lady Jay Dee akitumbuiza  mashabiki wa mji wa Kigoma na maeneo ya jirani katika uwanja wa Lake Tanganyika katika ziara ya wanamuziki waliofanya vizuri mwaka 2012 maarufu kama Kilimanjaro Music Tour 2013 iliyopewa kaulimbiu ya Kikwetu kwetu Jumamosi(Agost 31,2013).


Pro.Jay akitumbuiza na kupata shangwe kubwa toka kwa mashabiki wa mji wa Kigoma na maeneo ya jirani katika uwanja wa Lake Tanganyika (Jumamosi Agost 31,2013) kuwashuhudia wasanii wakali 12 waliopanda jukwaani katika ziara ya wanamuziki waliofanya vizuri mwaka 2012 maarufu kama Kilimanjaro Music Tour 2013 iliyopewa kaulimbiu ya Kikwetu kwetu.





Diamond na Wasafii wakitumbuiza na kupata shangwe kubwa toka kwa mashabiki. 


Picha Juu na Chini ni Muonekano wa mahudhurio ya maelfu ya wakazi wa mji wa Kigoma na maeneo ya jirani kufurika kwa wingi katika uwanja wa Lake Tanganyika kuwashuhudia wasanii wakali 12 waliopanda jukwaani katika ziara ya wanamuziki waliofanya vizuri mwaka 2012 maarufu kama Kilimanjaro Music Tour 2013 iliyopewa kaulimbiu ya Kikwetu kwetu.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad