Yanga SC yaanza Ligi kwa Kishindo cha 5-1 huku Arsenal ikiamka kwa kuiburuza Fulham 3-1 kwao. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 24, 2013

Yanga SC yaanza Ligi kwa Kishindo cha 5-1 huku Arsenal ikiamka kwa kuiburuza Fulham 3-1 kwao.



Shujaa wa Yanga SC Jerry Tegete.
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yana SC wameanza vema kampeni za kutetea taji lao, baada ya kuwafumua Ashanti United ‘Watoto wa Jiji’ mabao 5-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga leo(Agosti 24,2013) yalifungwa na Jerry Tegete dakika za 10 na 57, Simon Msuva dakika ya 47, Haruna Niyonzima dakika ya 73 na Nizar Khalfan dakika ya 90, wakati bao pekee la Ashanti lilifungwa na Shaaban Juma dakika ya 89.

Tegete alifunga bao la kwanza baada ya kupokea pasi ya nyota wa mchezo wa leo, Simon Msuva na kumlamba chenga beki Tumba Sued kabla ya kumtungua kipa Ibrahim Abdallah na lingine alifunga kwa krosi ya Msuva tena na kumvuta kipa kutoka langoni kabla ya kufunga.

Msuva alifunga bao bora zaidi katika mchezo huo, baada ya kuwalamba chenga mabeki wawili wa Ashanti, Tumba Sued na Ramadhani Malima kisha kuutumbukiza mpira kimiani kwa kichwa. 

Niyonzima alifunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na beki David Luhende na Nizar alifunga kwa krosi ya Frank Domayo wakati Juma aliipatia Ashanti bao la kufutia machozi baada ya kuwatoka mabeki wa Yanga. 

Kikosi cha Yanga SC:- kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Athumani Iddi ‘Chuji’/Frank Domayo dk18, Simon Msuva, Salum Telela, Didier Kavumbangu/Hussein Javu dk67, Jerry Tegete na Haruna Niyonzima. 

Ashanti United:- Ibrahim Abdallah, Khan Usimba, Emanuel Kichiba, Ramadhani Malima, Tumba Sued, Emanuel Memba, Fakih Hakika, Mussa Nampaka/Laurent Mugia dk61, Hussein Sued, Mussa Kanyaga/Shaaban Juma dk49 na Joseph Mahundi. 



Nako huko Katika Ligi kuu Nchini Uingereza - WAKICHEZA mapema hii leo kwenye Mechi ya Ligi Kuu England huko Craven Cottage, Arsenal waliifunga Fulham Bao 3-1 katika Mechi ya Dabi ya Jiji la London huku Lukas Podolski akiifungia Bao 2 katika mchezo huo.

Wakicheza kwa kasi kubwa kama ile iliyowapa ushindi wa Bao 3-0 huko Uturuki Juzi Jumatano walipoifunga Fenerbahce katika Mechi ya kwanza ya Raundi ya Mchujo ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, iliwachukua Dakika 14 kwa Arsenal kupiga Bao la kwanza kupitia Olivier Giroud.

Huku Mvua kubwa ikidondoka, Lukas Podolski alifunga Bao moja katika kila Kipindi na kufanya Gemu iwe 3-0 lakini Mchezaji mpya wa Fulham, Darren Bent, alifunga Bao pekee la Fulham baada ya kuunganisha pasi toka kwa Dimitar Berbatov.

Mechi inayofuata ya Ligi kwa Arsenal ni ya Nyumbani kwao Emirates hapo Septemba Mosi,mwaka huu ikiwa ni Dabi ya London ya Kaskazini dhidi ya Mahasimu wao Tottenham Hotspur.

VIKOSI:

Fulham: Stockdale, Riether, Hughes, Hangeland, Riise, Duff, Parker, Sidwell, Taarabt, Kasami, Berbatov.

Akiba: Ruiz, Kacaniklic, Karagounis, Briggs, Boateng, Etheridge, Bent.

Arsenal: Szczesny, Jenkinson, Sagna, Mertesacker, Gibbs, Rosicky, Ramsey, Walcott, Cazorla, Podolski, Giroud.

Akiba: Wilshere, Monreal, Fabianski, Sanogo, Frimpong, Gnabry, Zelalem.

Refa: Howard Webb 

 RATIBA YA LIGI KUU ENGLAND 2013/2014.


[SAA NI ZA BONGO] 

Jumapili 25 Agosti,2013.

18:00 Cardiff City v Manchester City

18:00 Tottenham Hotspur v Swansea City

Jumatatu 26 Agosti,2013.

22:00 Manchester United v Chelsea

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad