![]() |
Kaizer Chiefs FC. |
Azam FC imechapwa mabao 3-0 na wakongwe wa soka la Afrika Kusini,
Kaizer Chiefs.
Chiefs maarufu kama Amakosi wameifundisha soka Azam FC katika mechi ya
kirafiki iliyochezwa jijini Johannesburg.
Azam FC ilionyesha soka la ushindani, lakini Amakosi ambao walitumia
asilimia kubwa ya wachezaji ambao hukaa benchi walifanikiwa kuibuka na ushindi
huo kiulaini.
Mechi inayofuata na Azam FC ni Agosti 7 dhidi ya Mamelodi Sundowns
inayonolewa na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Pitso
Mosimane.
Baada ya hapo itashuka tena uwanjani kucheza na watukutu wa Afrika
Kusini Orlando Pirates siku ya Oktoba 13.
No comments:
Post a Comment