![]() |
Kwa
mbali ni Muonekano wa Daraja la Kimataifa la Rusumo linalotumika
kuunganisha nchi jirani za Rwanda na Tanzania na Ukivuka daraja hili upo nchi
jirani ya Rwanda.
|
![]() |
Ni Daraja la Kimataifa la
Rusumo linalotumika kuunganisha nchi jirani za Rwanda na Tanzania na Ukivuka
daraja hili upo nchi jirani ya Rwanda.
|
![]() |
Rusumo boda, mpakani mwa nchi jirani
za Rwanda na Tanzania.
|
![]() |
Rusumo boda, mpakani mwa nchi jirani za Rwanda na Tanzania. |
Tayari Serikali imesaini msaada wa shilingi bilioni
40 na serikali ya Japan kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa miradi miwili ya
maendeleo hapa nchini.
Waziri
wa Fedha na Uchumi Mustapha Mkulo amesema miradi hiyo ni ya ujenzi la wa daraja
la Rusumo litakalounganisha nchi ya Tanzania na Rwanda na upanuzi wa barabara
ya Kilwa ambapo itasaidia shughuli za maendeleo baina ya nchi hizo.
Pia
Benki ya dunia kupitia bodi yake ya utendaji imeidhinisha dola Milioni 340 kwa
ajili ya ujenzi wa mradi wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia nguvu za maji
kwenye maporomoko ya mto Rusumo ulioko ukanda wa maziwa makuu barani
Afrika.
Mradi huo unalenga kunufaisha wakazi Milioni 62 walioko Burundi, Rwanda
na Tanzania na unafuatia ziara ya Rais wa Benki ya dunia Jim Yong Kim na Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwenye ukanda huo mwezi Mei mwaka huu.
Colin
Bruce ambaye ni Mkurugenzi wa mikakati na operesheni kwenye Benki ya dunia
amesema kukamilika kwa mradi huo kutatoa hakikisho la upatikanaji wa umeme,
kutapunguza gharama za umeme na kuchochea shughuli za kiuchumi zitakazowezesha
kuongeza upatikanaji wa ajira.
Amesema
uhaba wa umeme kwenye eneo hilo ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ambapo ni
asilimia nne tu ya wananchi wa Burundi wanapata huduma ya umeme ilhali Rwanda
ni asilimia 13 na Tanzania ni asilimia 15.
No comments:
Post a Comment