Michuano ya
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2013/2014 inaanza kutimua vumbi Leo
(Agosti 24 mwaka huu) katika viwanja saba tofauti huku mabingwa watetezi Yanga
wakianza kutetea ubingwa wao kwa kuikaribisha Ashanti United kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Uwanja wa
Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Azam
ya Dar es Salaam na wenyeji Mtibwa Sugar. Oljoro JKT itaikaribisha Coastal
Union kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.
Mgambo
Shooting itaoneshana kazi na JKT Ruvu ambayo hivi sasa iko chini ya Kocha
Mbwana Makata. Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati Rhino
Rangers itakwaruzana na Simba katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Mbeya City
iliyopanda VPL msimu huu itapimana ubavu na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya huku Ruvu Shooting ikiialika Mabatini,
Mlandizi timu ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya.
Mzunguko wa
pili wa ligi hiyo utachezwa Agosti 28 mwaka huu. Baada ya hapo ligi itasimama
kupitisha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Gambia na Tanzania (Taifa
Stars) itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul. VPL itaingia mzunguko
wa tatu Septemba 14 mwaka huu.
MECHI ZA UFUNGUZI:-Jumamosi Agosti 24,2013.
YANGA | v | ASHANTI UNITED | UWANJA WA TAIFA | DSM |
MTIBWA SUGAR | v | AZAM FC | MANUNGU | MOROGORO |
JKT OLJORO | v | COASTAL UNION | SH. AMRI ABEID | ARUSHA |
MGAMBO JKT | v | JKT RUVU | MKWAKWANI | TANGA |
RHINO RANGERS | v | SIMBA | A.H. MWINYI | TABORA |
MBEYA CITY | v | KAGERA SUGAR | SOKOINE | MBEYA |
RUVU SHOOTINGS | v | PRISONS | MABATINI | PWANI |
LIGI KUU
ENGLAND: JUMAMOSI 24,2013-DABI YA LONDON.
CRAVEN COTTAGE itashuhudia Dabi ya Jiji la London wakati Fulham watakapoikaribisha Arsenal katika Mechi ya mapema kabisa ya Ligi Kuu England kuchezwa Jumamosi Agosti 24,2013.
Baada ya Mechi hii ya Dabi, zitafuata Mechi nyingine 6 za Ligi hiyo hiyo Jumamosi huku Jumapili kuchezwa Mechi 2 na Jumatatu ni ule mtanange mkali huko Old Trafford kati ya Mabingwa Manchester United na Chelsea.
Kwenye Dabi ya London huko Craven Cottage, Fulham inatinga kwenye Mechi hii ikiwa imeshinda Mechi yao ya kwanza ya Ligi walipoishinda Sunderland ugenini kwa Bao 1-0 Wikiendi iliyopita ambayo pia Arsenal walianza Msimu wao wa Ligi kwa kucheza Nyumbani Uwanjani Emirates na kuchapwa Bao 3-1 na Aston Villa.
Lilikuwa pigo kubwa kwa Arsenal na Meneja wao Arsene Wenger lakini walijizoa na Juzi Jumatano huko Instanbul, Uturuki, walicharuka na kuinyuka Fenerbahce Bao 3-0 katika Mechi ya kwanza ya Raundi ya Mchujo ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Hali hii inafanya Dabi hii iwe Mechi ya mvuto kwa Wadau wa Soka.
Hull City, chini ya Meneja Steve Bruce, Gwiji wa zamani wa Man United, ambao Wikiendi iliyopita walianza Ligi kwa kuchapwa 2-0 na Chelsea huko Stamford Bridge, watakuwa Nyumbani KC Stadium kuwakaribisha Norwich City waliotoka 2-2 na Everton katika Mechi yao ya kwanza.
Wapya kwenye Ligi Kuu, Crystal Palace, baada ya kufungwa 1-0 na Tottenham Hotspur, watasaka ushindi wao wa kwanza wakiwa Ugenini kucheza na Stoke City ambayo pia ilifungwa huko Anfield Bao 1-0 na Liverpool.
Newcastle, baada ya kunyukwa 4-0 na Man City huko Etihad, watakuwa Nyumbani St James Park kucheza na West Ham iliyoifunga Crdiff City Bao 2-0.
Huko Goodison Park, Everton, baada ya kutoka 2-2 na Norwich, itataka kuichapa West Bromwich Albion iliyoanza Ligi kwa kichapo cha Nyumbani cha Bao 1-0 toka kwa Southampton.
Nao Southampton watakuwa Nyumbani kuikaribisha Sunderland iliyoanza kwa kufungwa kwao Stadium of Light Bao 1-0 na Fulham.
Mechi ya mwisho kwa Jumamosi ni ile itakayochezwa Villa Park kati ya Aston Villa na Liverpool.
Hii ni mechi ya tatu kwa Aston Villa ambao walianza Ligi Jumamosi iliyopita kwa kuifunga Arsenal 3-1 na kufungwa 2-1 na Chelsea, Mechi zote wakiwa wamecheza Ugenini.
RATIBA LIGI KUU
ENGLAND
[SAA NI ZA BONGO]
Jumamosi 24 Agosti,2013.
17:00 Everton v West Bromwich Albion
17:00 Hull City v Norwich City
17:00 Newcastle United v West Ham United
17:00 Southampton v Sunderland
17:00 Stoke City v Crystal Palace
19:30 Aston Villa v Liverpool
Jumapili 25 Agosti,2013.
18:00 Tottenham Hotspur v Swansea City
Jumatatu 26 Agosti,2013.
22:00 Manchester United v Chelsea
SERIE A KUANZA
WIKIENDI HII, JUVE KUTAWALA??
MABINGWA watetezi Juventus Jumamosi Usiku
watatinga dimbani kuanza utetezi wa Taji laokatika Mechi ya kwanza ya Ligi
Serie A kwa Msimu wa 2013/14 huku Ligi hiyo ikiwa imegubikwa na Skandali za
kupanga matokeo Mechi na vitendo vya Ubaguzi.
Mechi ya kwanza kabisa ya Ligi itachezwa mapema Jumamosi kabla ya ile ya Juventus na itakuwa kati ya Timu iliyopanda Daraja Hellas Verona na AC Milan.
DONDOO MUHIMU:
TIMU ZILIZOPANDA DARAJA KUINGIA SERIE A:
-Livorno
-Sassuolo
-Hellas Verona
MAKOCHA WAPYA:
-Rafael Benitez (Napoli)
-Giuseppe Sannino (Chievo)
-Rudi Garcia (AS Roma)
-Fabio Liverani (Genoa)
-Walter Mazzarri (Inter Milan)
Juventus wataingia kwenye Mechi na Sampdoria wakiwa tayari wameshatoa onyo kali kuhusu Msimu huu mpya baada ya kutwaa Supercup kwa kuinyuka Lazio Ba0 4-0 Jumapili iliyopita huku Mchezaji wao mpya, Carlos Tevez, waliemnunua kutoka Manchester City, aking’ara na kufunga Bao moja.
SERIE A
RATIBA-Mechi za Kwanza
[Saa za Bongo]
Jumamosi Agosti 24,2013.
21:45 Sampdoria v Juventus
Jumapili Agosti 25,2013.
19:00 Internazionale v Genoa
21:45 SS Lazio v Udinese
21:45 Parma v Chievo Verona
21:45 Torino FC v Sassuolo
21:45 Napoli v Bologna
21:45 Livorno v AS Roma
21:45 Cagliari v Atalanta
Jumatatu Agosti 26,2013.
21:45 Fiorentina v Catania
Mechi hiyo ya Supercup kati ya Juventus na Lazio ilionyesha waziwazi matatizo makubwa ya Soka la Italy hivi sasa kufuatia vitendo vya Kibaguzi toka kwenye Majukwaa ya Watazamaji na pia kukosekana kwa Nahodha wa Lazio, Stefano Mauri, ambae anatumikia Kifungo cha Miezi 6 kwa kuhusishwa na upangaji matokeo Mechi.
Pamoja na matatizo hayo, Serie A pia inakabiliwa na matatizo ya kuwa na Viwanja vichakavu, matatizo ya Fedha na kila aina ya uhuni Viwanjani vitu ambavyo vimeikosesha sifa na kufanya Wachezaji wengi kupendelea kwenda kucheza Spain, England na, siku hizi, kuelekea Germany na France.
Hata hivyo, Msimu huu mpya wapo Nyota kadhaa waliotua Italy wakitokea nje na hao ni pamoja na Tevez, alietua Juve, Gonzalo Higuain aliekwenda Napoli na Mjerumani Mario Gomez alienunuliwa na Fiorentina.
Msimu uliopita Kocha wa Juventus Antonio Conte alisema kuwa itachukua Miaka mingi kwa Klabu ya Italy kuweza kutwaa tena Kombe la UEFA CHAMPIONZ LIGI.
No comments:
Post a Comment