Taswira ya Mkutano wa Mabaraza huru ya Katiba ya CHADEMA wilayani Ngara Mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, August 20, 2013

Taswira ya Mkutano wa Mabaraza huru ya Katiba ya CHADEMA wilayani Ngara Mkoani Kagera.

Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ,Mwenyekiti wa Chadema Bw Freeman Mbowe, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema na Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Bw John Mnyika na Bw.Tundu Lisu wakijiandaa kutua katika uwanja wa posta ya zamani Mjini Ngara (Agost 17,2013) kushiriki mkutano wa baraza huru la wazi la Katiba ya Chama hicho kwa wakazi wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera,lililoandaliwa na chama hicho.




Toka kushoto ni Mbunge Anton Mbasa,Mwenyekiti wa Chadema Bw Freeman Mbowe, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema na Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Bw John Mnyika wakiondoka  katika uwanja wa posta ya zamani Mjini Ngara (Agost 17,2013) baada ya kumalizika  mkutano wa baraza huru la wazi la Katiba ya Chama hicho kwa wakazi wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera,lililoandaliwa na chama hicho.




Muonekano wa Wanachama wapya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema waliojiunga ,wakitoka Vyamba vya CCM na NCCR-Mageuzi na kukabidhiwa Kadi na Mwenyekiti wa Chadema Bw Freeman Mbowe, wakati wa mkutano wa baraza huru la wazi la Katiba ya Chama hicho kwa wakazi wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera,lililoandaliwa na chama hicho.



Gari la Radio Kwizera lenye Matangazo ya Nje PA (Lililokodiwa na Chadema) likiendelea na Matangazo yake uwanjani hapo katika mkutano wa baraza huru la wazi la Katiba ya Chama hicho kwa wakazi wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera, (Kwa mahitaji ya Matangazo na Vifaa Vyake fika Ofisi za radio Kwizera-Ngara) upate kwa bei nafuu kabisa kwa ajili ya sherehe na Mikutano ya Vyama mbalimbali vya Siasa).

Wananchi ,Wapenzi na Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)wakipitisha maoni yao wakati wa mkutano wa baraza huru la wazi la Katiba ya Chama hicho kwa wakazi wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera,lililoandaliwa na chama hicho(Agosti 17,2013).
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimetoa wito kwa Watanzania kuunga mkono rasimu ya katiba mpya iliyoratibiwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Jaji Mstaafu Joseph Warioba.

Mwenyekiti wa Chadema Bw Freeman Mbowe alitoa wito huo (Agost 17,2013) wakati wa mkutano wa baraza huru la wazi la Katiba ya Chama hicho kwa wakazi wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera,lililoandaliwa na chama hicho.

Bw.Mbowe alisema kwa asilimia kubwa rasimu ya katiba inayoendelea kujadiliwa imezingatia mambo makuu ya kitaifa hasa muundo wa serikali kwa kupendekeza kuwepo na serikali 3.

Aidha Mwenyekiti huyo Taifa wa CHADEMA amewataka Watanzania kuhakikisha Kiswahili kinakuwa Lugha rasmi ya Taifa katika katiba ijayo na kwamba Kiingereza linapaswa kuwa somo la lazima kuanzia elimu ya awali hadi elimu ya juu ili kuwaandaa kwa usawa Watanzania wote katika ushindani wa ajira baada ya kuhitimu masomo yao.

Nae mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema na Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Bw John Mnyika ameitaka Wizara ya Katiba na Sheria kuhakikisha inachapisha na kusambaza nakala za Rasimu ya Katiba mpya nchini Kote ili Watanzania waisome na kutoa maoni sahihi ili kupata Katiba bora.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera waliotoa maoni yao mbele ya viongozi hao wa Chadema wamependekeza kuwa Katiba ijayo itamke bayana kuhusu haki ya Demokrasia ya Vyama vingi,Utawala wa Sheria na Haki za Binadamu pamoja na Wananchi kumiliki Rasilimali na Maliasili za taifa na Kunufaika nazo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad