Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa imejadili na kutolea maamuzi pamoja na mambo
mengine suala la Madiwani wanane waliotangazwa kufukuzwa uanachama na
Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera.
Katika
maamuzi yake, Kamati Kuu imebatilisha uamuzi uliofanywa na Halmashauri Kuu CCM
ya Mkoa wa Kagera Agosti 13, 2013 wa kuwafukuza uanachama Madiwani hao.
Hivyo
Madiwani hao wanane ni wanachama halali wa CCM.
Kamati Kuu imetoa uamuzi huo, baada ya kubaini
kuwa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera haikuzingatia Katiba ya CCM ya 1977
Toleo la 2012 Ibara ya 93 (15).
Ibara
hiyo inasomeka kuwa moja ya kazi ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa ni:-
“Kumwachisha au kumfukuza uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa mwisho
unafanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa, isipokuwa kwa suala la kumvua
uanachama au uongozi Diwani lisifanyike hadi Kamati Kuu imearifiwa na kutoa
maelekezo”.
![]() |
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Kagera Constansia Muhiye na Katibu wa CCM wa mkoa huo, Abedi
Mushi wakisubiri kuingia ukumbini kukutana na Kamati kuu mjini Dodoma .
|
Aidha,
Kamati Kuu imewaonya Madiwani wa CCM wa Manispaa ya Bukoba, Mbunge wa Bukoba
Mjini na Meya kwa kusababisha kukosekana kwa utulivu, mshikamano na amani
katika Manispaa na Chama.
Kamati
Kuu pia imeitaka Serikali kumwagiza mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali(CAG)
kufanya ukaguzi maalum wa haraka wa mambo yanayolalamikiwa dhidi ya Meya ili
ukweli ujulikane na matokeo ya uchunguzi huo yasilishwe kwenye baraza la
madiwani ili hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria na taratibu
zinazoongoza Serikali za Mitaa.
![]() |
Katibu wa Itikadi na
Uenezi
-CCM Nape Nnauye.
|
Wakati
tuhuma hizo dhidi ya Meya zikichunguzwa; Kamati Kuu inawataka Madiwani wa CCM
kurejesha utulivu kwenye Manispaa na Chama kwa ujumla ili kufanikisha
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuwaletea maendeleo wananchi wa
Bukoba.
Katika
hatua nyingine Mtikisiko mkubwa umekikumba Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya
kubariki kufukuzwa uanachama kwa Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, Mansoor
Himid Yussuf.
Mbali
ya uamuzi huo, CCM imefanya mabadiliko mengi katika jumuiya zake za Umoja wa
Vijana (UVCCM) na Jumuiya ya Wazazi.
Uamuzi
wa kufukuzwa Mansoor uanachama, umehitimisha safari ya mwanasiasa huyo mwenye
ushawishi visiwani Zanzibar kupoteza rasmi uwakilishi wa jimbo.
Mansoor,
amekuwa miongoni mwa Wazanzibari walio mstari wa mbele kutetea muundo wa
Muungano, utakaoipa Zanzibar mamlaka kamili ya dola.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana(Agosti 27,2013), Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi
na Uenezi Nape Nnauye alisema kikao cha NEC, kilijadili kwa kina tuhuma dhidi
ya mwakilishi huyo na kutoka na uamuzi wa kumfukuza uanachama wa CCM.
Alisema
NEC, ilipokea masuala mbalimbali yakiwemo maamuzi ya Kamati maalumu ya CCM
Zanzibar dhidi ya Mansoor, ikiwemo kushindwa kusimamia malengo ya chama na
kutekeleza masharti ya uanachama.
Tuhuma
kubwa iliyowasilishwa mbele ya NEC, ni pamoja na kudaiwa kushindwa kutekeleza
wajibu wa mwanachama na kukiuka maadili ya kiongozi.
Mbali
na hilo, ilielezwa ameikana ilani ya CCM ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010-2015 na
kukisaliti chama.
Kutokana
na hali hiyo, Nape alisema baada ya kujiridhisha vya kutosha na tuhuma dhidi ya
Mansoor, NEC iliridhia uamuzi wa kumfukuza uanachama.
“Yapo
mambo mengi ambayo NEC imejadili katika kikao chake ikiwemo suala la Katiba
Mpya, mgogoro wa umeya Bukoba ambapo hadi sasa bado haujamalizika.
“Mbali
na hilo, NEC imeridhia kufukuzwa kwa uanachama kwa Mansoor na kuanzia leo
(jana) si kiongozi tena wa CCM,” alisema Nape.
Sakata
la Mansoor la kufukuzwa kwake uanachama, lilianza katika kikao cha Kamati
Maalumu iliyoketi Agosti 18, mwaka huu na kutoka na azimio la kumvua uanachama
Mwakilishi huyo wa Kiembesamaki ambaye alidaiwa kukiuka maadili ya chama hicho.
Katika
kikao hicho, Mansoor amekuwa akipingana na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka
2010, inayoamini katika muundo wa Serikali mbili.
Kwa
mara ya kwanza, tuhuma za Mansoor zilifikishwa katika kikao cha Kamati ya
Maadili ya CCM Zanzibar, kilichoketi Agosti 16, 2013 katika Ofisi za CCM
Kisiwandui ambapo wajumbe wa kamati hiyo kwa kauli moja walitoka na azimio la
kumfuta uanachama mwakilishi huyo.
Dk.
Shein ndiye aliyeongoza kikao cha Kamati ya Maadili, huku wajumbe wakiwa ni
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, Mohamed Hija, Mbaruk Rashid
Omari na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd.
Kwenye
kikao cha Mkoa wa Mjini Magharibi, Mansoor alitoa utetezi wake na kusema kuwa
kama kufungwa afungwe, kama kunyongwa anyongwe na kama kufukuzwa afukuzwe,
lakini anataka Serikali ya mkataba.
UTEUZI.
Kikao
cha Halmashauri Kuu pia kimeridhia, uteuzi wa Makatibu wateule wapya wa Jumuiya
za CCM, za Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuia ya Wazazi na Umoja wa
Wanawake Tanzania (UWT).
Katika
uteuzi huo mapendekezo hayo yaliyofanywa na Kamati Kuu ya CCM na kuridhiwa na
NEC, kwa upande wa UVCCM ameteuliwa aliyekuwa Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa
Morogoro, Sixtus Mapunda na kwa upande wa Jumuia ya Wazazi ni Mjumbe wa NEC
kutoka Pemba, Seif Shabani Mohamed, huku kwa upande wa UWT akiachwa Katibu Mkuu
wa sasa, Amina Makilagi.
Mapunda
atachukua nafasi iliyokuwa imneshikiwa na Martine Shigela ambaye ameongoza
UVCCM kwa miaka mitano sasa, na Seif Shabani Mohammed kutoka Pemba akichukua
nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Hamis Suleiman Dadi ambaye pia amekuwa katika
wadhifa kwa miaka mitano sasa.
Pia,
NEC imeridhia mapendekezo ya Kamati Kuu
kwa ajili ya kuziba nafasi Makatibu wa CCM wa mikoa mitatu ya Morogoro,
Kaskazini Pemba na Geita ambayo kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa imekuwa wazi
kwa muda mrefu sasa kutrokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo.
Kufuatia
mapendekezo hayo ya Kamati Kuu, ambayo yameridhiwa na NEC, walioteuliwa na
mikoa yao ikiwa kwenye mabano ni Msaidizi Kitengo cha Uchaguzi, CCM Ofdisi Ndogo ya Makao Makuu ya
CCM, Romuli Rojas John (Morogoro), aliyekuwa Katibu Katibu wa wilaya ya Mkinga,
Kassim Mabrouk Mbarak (Kaskazini Pemba) na aliyekuwa Katibu wa CCM Igunga, Mary
Maziku (Geita).
Taarifa
Rasmi ya CCM ya majina ya Makatibu wa Wilaya walioteuliwa na NEC
Ndugu
Ashura Amanzi
Ndugu
Rukia Saidi Mkindu
Ndugu
Elias J. Mpanda
Ndugu
Jonathan M. Mabihya
Ndugu
Mulla Othman Zuberi
Ndugu
Jumanne Kapinga
Ndugu
Ali Haji Makame
Ndugu
Jacob G. Makune
Ndugu
Juma A. Mpeli
Ndugu
Hawa Nanganjau
Ndugu
Abdulrahman Shake
Ndugu
Subira Mohamed Ameir
Ndugu
Abdallah Shaban Kazwika
Ndugu
Juma Bakari Nachembe
Ndugu
Josephat Ndulango
Ndugu
Rajab Uhonde
Ndugu
Abeid Maila
Ndugu
Mohamed Lawa
Ndugu
Mariam Sangito Kaaya
Ndugu
Bakar Lwasa Mfaume
Ndugu
Julius Peter
Ndugu
Jumanne Kitundu Mginga
Ndugu
Mathias Nyombi
Ndugu
Mohamed Hassan Moyo
No comments:
Post a Comment