Kamanda Kalangi alisema Rwesheleka alipita katika kizuizi cha
polisi cha Chanyamisa saa 11:00 jioni akisema kuwa anaelekea katika kijiji cha
Nyakasimbi kumuona bibi yake ambaye alidai ni mgonjwa.
Kwamba saa 2:00 usiku wakati diwani huyo akirudi Chonyonyo
alikutana na mtu mmoja ambaye alimsimamisha na kisha kumtisha kwa kumuonyesha
bastola na kumwamuru ageuze gari na kurudi barabara ya Benako.
Alisema kuwa wakati akiendelea na safari kuelekea alikoelekezwa,
mbele kidogo walikutana na watu wengine wawili na kisha akaamriwa asimamishe
gari na watu hao walianza kupakiza mizigo ndani.
Kamanda aliongeza kuwa wakati watu hao wakiendelea kupakiza
mizigo ndani ya gari, diwani huyo alifanikiwa kuwatoroka na kutokomea porini na
baadaye katika barabara iendayo Karagwe ndipo ghafla likatokea gari aina ya
Toyota Hiace likitoka Benako na kumpa msaada.
Alisema kuwa wakati akiwa kwenye Hiace aliambiwa na wasafiri
kuwa wameona gari lake likiwaka moto maeneo ya Nyakasimbi.
Kalangi alisema kuwa diwani Rwesheleka alifika katika kituo
kidogo cha polisi Chanyamisa saa 3.30 usiku kutoa taarifa kuwa alitekwa na
majambazi.
“Baada ya kutoa taarifa, polisi waliondoka naye mpaka eneo la
tukio na kukuta gari hilo likiendelea kuteketea. Bado uchunguzi unaendelea
kwani mazingira yake yanatatanisha.
Rwesheleka alipohojiwa na gazeti hili jana, alisema alinusurika
kifo wakati akitoka kumuona bibi yake eneo la Nyakasimbi.
No comments:
Post a Comment